Saturday, December 22, 2012

Wanawake ni chanzo cha matatizo ya nguvu za kiume

Wanawake ni chanzo cha matatizo ya nguvu za kiume WIKI hii mpenzi msomaji wangu nitazungumzia tat... thumbnail 1 summary

Wanawake ni chanzo cha matatizo ya nguvu za kiume

WIKI hii mpenzi msomaji wangu nitazungumzia tatizo la nguvu za kiume ambalo limekuwa likiwasumbua wanaume wengi walio kwenye ndoa na wale walio kwenye uhusiano wa kawaida.
Hii imesababisha baadhi yao kuhangaika huku na kule kutafuta dawa na hata wanapofanikiwa wanajikuta wakiendelea kuwa na tatizo hilo.
Kwa kifupi ni tatizo linalozisumbua ndoa nyingi kwani mwanaume yeyote anayejijua ni rijali anapokumbwa na tatizo hili hukosa hali ya kujiamini na kumfanya asiwe na amani na wakati mwingine kuhisi hastahili kuwa na mke.
Kama wewe ni mfuatiliaji wa makala za ndoa na uhusiano utabaini kuwa, tatizo la nguvu za kiume limekuwa likielezwa kuwa linasababishwa kwa kiasi kikubwa na vyakula tunavyokula lakini uchunguzi umebaini kuwa, wanawake wanachangia kwa kiasi kikubwa katika hili.
Mwandishi mmoja wa habari za kijamii wa Uingereza, Johnson Fredrick aliwahi kueleza kwa kina kwamba wanawake wamekuwa chanzo kikubwa cha wanaume kupungukiwa na nguvu za kiume kama ifuatavyo:
Karaha za mwanamke
Anaeleza kuwa, karaha za wanawake kwa waume zao ni chanzo kikubwa sana cha upungufu wa nguvu za kiume. Kama mwanamke atakuwa si mstaarabu kwa mumewe na akawa ni mtu wa kuropoka lolote linalomjia kinywani mwake bila kuwa na staha, humfanya mumewe kuingiza akilini mwake kitu ambacho humuathiri watakapokuja kukutana faragha.
Chukua mfano kwamba, mwanamke anatibuana na mumewe kisha anambwatukia kwa kumwambia; ‘we mwanaume gani… huna lolote wewe ni mwanaume suruali tu.’
Maneno kama haya hayawezi kumfurahisha mwanaume na akiyaweka akilini mwake hata siku akija kukutana na mkewe kwenye uwanja wao wa kujidai kisha yakamjia, ni vigumu sana kupata ile nguvu na msisimko wa kufanya tendo kwa ufasaha.
Ndiyo maana utashangaa mwanaume aliyekutana na hali hiyo atakapojaribu kutoka nje ya ndoa yake na kwenda ‘kuduu’ na mwanamke mwingine, anaweza kuwa na nguvu za ajabu na kujikuta akilifurahia tendo tofauti na na inavyokuwa kwa mkewe.
Usaliti
Mtaalam huyo wa masuala ya mapenzi anaeleza kuwa, mwanamke ambaye ‘hajatulia’ ni rahisi sana kumfanya mume wake kukosa nguvu za kiume. Hii inakujaje? Hakuna kitu kinachouma kama kuibiwa penzi lako na mwanamke anapokuwa mrahisi wa kusaliti humfanya mumewe kuumia moyoni na hatimaye kukosa msisimko katika tendo la ndoa.
Kukosekana utundu na ubunifu
Ukijaribu kufuatilia kwa makini utagundua baadhi ya wanawake walio kwenye uhusiano, hasa ndoa si watundu na hawana ubunifu wawapo faragha na wapenzi wao. Tabia hii humfanya mwanaume awe mhimili wa pekee katika zoezi zima na pale atakapochoka hawezi kupata sapoti kutoka kwa mwenza wake, matokeo yake ni mchezo kuishia hapo.
Lakini endapo mwanamke naye anayajua mambo, atakuwa na uwezo wa ‘kumbusti’ mpenzi wake na hatimaye kufika pale walipotarajia.
Tambo zisizofaa
Kuna wanawake ambao hutumia lugha za kujitamba sana kabla ya kukutana faragha na waume zao bila kujua madhara ya baadaye. Unakuta mwanamke anamwambia mumewe maneno haya:
‘Baby leo ukirudi nitakupa mambo adimu ambayo huwezi kuyapata kwingine, wewe jiandae kwa libeneke maana ngoma ya leo haitakuwa na simile’.
Unaweza kumwambia maneno hayo mumeo kwa nia njema tu ili kumfanya arudi mapema kuwahi hivyo vinono ulivyomuandalia lakini kisaikolojia huleta mazingira ya hofu ambayo yanaweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.
Mwanamke kutokuwa nadhifu
Kuna msemo huko uswahilini usemao; mwanamke ni mazingira. Siyo uongo! Mwanamke anatakiwa kuwa msafi wa mwili na nguo hasa pale anapokuwa karibu na mpenzi wake.
Kisaikolojia mwanamke msafi ni rahisi sana kumshawishi mume wake kukutana naye faragha na hata wanapokuwa wanafanya mambo yao, msisimko huwa mkubwa.
Lakini endapo mwanamke atakuwa hajijali, anaweza kumsababishia mume wake matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume. Hakuna asiyefahamu umuhimu wa usafi wa mwili na kero za uchafu wakati wa tendo, hivyo ni wazi kuwa mwanamke akiwa mchafu atamfanya mwanaume apoteze msisimko na uwezo wa tendo la ndoa.
Kwa hiyo usafi wa mwili na nguo kwa mwanamke ni muhimu sana ili kuweza kuboresha maisha ya kimapenzi.
Kwa leo nilidhamiria kuwaandikia hayo nikiamini ukiyafanyia kazi yatakuwa ni yenye manufaa kwako na mpenzi wako.

Wednesday, December 12, 2012

VODACOM YASHAURI VILABU LIGI KUU KUIMARISHA VIKOSI KUPITIA DIRISHA DOGO

VODACOM YASHAURI VILABU LIGI KUU KUIMARISHA VIKOSI KUPITIA DIRISHA DOGO Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Ke... thumbnail 1 summary

VODACOM YASHAURI VILABU LIGI KUU KUIMARISHA VIKOSI KUPITIA DIRISHA DOGO

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa akiongea na wanahabari (hawapo pichani).
Dar es Salaam, 12. Des. 2012 … Mdhamini wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara, Kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania imezishauri klabu zinazokipiga ligi kuu kutumia nafasi ya usajili wa dirisha ndogo kuimarisha vikosi ili kuongeza kasi ya ushindani katika mzunguko wa lala salama wa ligi hiyo.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na kampuni hiyo, Vodacom imesema vuilabu vina nafasi ya kutumia fursa ya dirisha dogo la usajili kujihakikishia kufanya vema kuelekea ubingwa wa ligi kuu.
“Msimamo wa ligi sasa unaonyesha dhahiri kuwa hata timu iliyo katika nafasi ya tano ina nafasi ya kuchukua ubingwa ikitambua mapema mapungufu yaliyosababisha usifanye vizuri katika mzunguko wa kwanza kupitia dirisha dogo klabu inaweza kujisahihisha.” Amesema Kelvin Twissa, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania.
“Kabla ya usajili wa dirisha ndogo haujafanyika ni vyema klabu zikafanya tathmini ya aina ya wachezaji wanaohitaji na kufanya usajili wa kisayansi ambao utazijenga timu na kukabiliana na mikiki ya msimu ujao ambao ni mgumu zaidi,” amesema Twissa.
“Tumeshuhudia ushindani wa kiwango cha juu katika mzunguko wa kwanza hili linaweza kuufanya mzunguko wa pili ukawa mgumu zaidi kuusaka ubingwa na kujinusuru kushuka daraja hivyo ni vema kila timu ikajiandaa kimkakati kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa ligi”Aliongeza Twissa
Mkuu huyo wa Masoko amesema kuwa kampuni yake inaendelea kutekeleza dhamira yake ya kuinua michezo na wao kama wadhamini wa ligi kuu ni vyema kushirikiana na timu ili kujenga uwezo na kiwango cha soka nchini.
“Timu zetu zimekuwa gumzo katika michuano ya Chalange kwa kufunga magoli mengi zaidi na kuonyesha kiwango cha hali ya juu. Ni Wachezaji hao hao wanaocheza katika Ligi kuu ya Vodacom pamoja na wale wa ligi kuu Zanzibar ndio wamezua gumzo katika michuano hiyo,” amesema Twissa, na kuongeza kuwa, “Ukitazama hilo kwa kina lazima utawapa makocha wetu wa Tanzania sifa kwani ndio wanao waandaa wachezaji katika ngazi ya vilabu na wanapokuja kucheza katika timu ya taifa wanakuwa na mafanikio makubwa,”
Twissa amehitimisha kwa kuzisihi timu za Simba na Azam kufanya maandalizi ya michuano ya kimataifa inayo wakabili na kuzitakia kila la kheri.
“Tunazitakia kila la kheri timu zitakazoiwakilisha nchi yetu katika michuano ya kimataifa. Tunaamini tutafika mbali kwani ligi yetu inaendelea kuwa bora zaidi,” amesema Twissa.
Klabu ya Simba itachuana na timu ya C.R Libolo ya Angola katika michuano na Klabu bingwa Afrika na Azam FC itachuana na Ali Nasir Juba ya Sudan Kusini katika kombe la Shirikisho.

RAIS WA ZAMANI WA MADAGASKA MARC RAVALOMANANA AMEKUBARI KURUDI NCHINI KWAKE

RAIS WA ZAMANI WA MADAGASKA MARC RAVALOMANANA AMEKUBARI KURUDI NCHINI KWAKE Rais Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akiwa na Rais wa zamani... thumbnail 1 summary

RAIS WA ZAMANI WA MADAGASKA MARC RAVALOMANANA AMEKUBARI KURUDI NCHINI KWAKE

Rais Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akiwa na Rais wa zamani wa Madagascar , Marc Ravalomanana wakati wa mkutano na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es Salaam jana Desemba 11, 2012.
(PICHA NA IKULU)
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete amefanikiwa kufanya mazungumzo na Rais wa zamani wa Madagaska Marc Ravalomanana ambaye amekubari kurudi nchini kwake baada ya kuwa uhamishoni  nchini  Afrika Kusini tangu mwaka 2009.
Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari Ikulu jijini Dar es Salaam leo,  Raisi Kikwete amesema Ravalomanana amekubali pia kutokugombea katika uchanguzi utakaofanyika nchini humo mwezi Mei 2013 ili kuleta amani na utulivu.
“Nimezungumza na Rais Ravalomanana na amekubali kurudi nchini kwake madagaska  na kukubali kutokukugombea  uchaguzi ujao kama maamuzi ya  Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) yalivyofikiwa katika vikao vyake vya hivi karibuni”, amesisitiza Rais Kikwete.
Raisi kikwete amefafanua  kuwa Ravalomanana  anarudi nchini Madagaska bila masharti yoyote na atapewa ulizi na Serikali ya nchi hiyo ikisaidiana na Jumuiya ya SADC.
Kwa upande wake Rais Ravalomanana amemshukuru Rais kikwete kwa kufanikisha mazungumzo hayo  na  amesema anaheshimu maamuzi yaliyotolewa na SADC kwa lengo la kuisaidia Madagaska kuwa katika hali ya amani.
“Ninamshukuru Rais Kikwete kwa kufanikisha mazungumzo haya na niko tayari kurudi nchini kwangu kujenga, kuimarisha na kushirikiana na wananachi  ili kuleta amani na utulivu,” amesema  Ravalomanana.
Rais kikwete alipewa jukumu na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika  la kufanya mazungumzo na Marais wote wa wawili,  Rais wa sasa wa Madagaska Andry Rajoelina na Rais wa zamani Marc Ravalomanana ambapo mazungumzo bado yanaendelea kwa upande wa Rais Rajoelina.
Dar es Salaam

Wednesday, December 5, 2012

TANZANITE AMSHUTUMU DIMOND KWAMBA AMEMROGA

                TANZANITE : DIAMOND ANANIROGA                                                                                        ... thumbnail 1 summary
               

TANZANITE : DIAMOND ANANIROGA

                                                                    
Na Hamida Hassan

MWANAMUZIKI, Mwingereza Athuman ‘Tanzanite’ ameibuka na madai mazito kuwa, eti msanii mwenzake Nasibu Abdul ‘Diamond’ amemroga.
Mwingereza Athuman ‘Tanzanite’.
Akizungumza katika kituo kimoja cha redio jijini Mwanza hivi karibuni, Tanzanite alidai kuwa aliugua sana kifua ambapo alifikia hatua ya kutoa makohozi yenye damu yaliyochanganyika na nywele.

“Nilikwenda hospitali lakini hali ilizidi kuwa mbaya, tukageukia kwa waganga wa kienyeji, lakini kila sehemu tuliyokuwa tukienda tulikuwa…

Na Hamida Hassan
MWANAMUZIKI, Mwingereza Athuman ‘Tanzanite’ ameibuka na madai mazito kuwa, eti msanii mwenzake Nasibu Abdul ‘Diamond’ amemroga.
Mwingereza Athuman ‘Tanzanite’.
Akizungumza katika kituo kimoja cha redio jijini Mwanza hivi karibuni, Tanzanite alidai kuwa aliugua sana kifua ambapo alifikia hatua ya kutoa makohozi yenye damu yaliyochanganyika na nywele.
“Nilikwenda hospitali lakini hali ilizidi kuwa mbaya, tukageukia kwa waganga wa kienyeji, lakini kila sehemu tuliyokuwa tukienda tulikuwa tukitajiwa jina la Nasibu kuwa ndiye aliyenifanyia ‘mandingo’.
“Nilikuwa sitaki kuamini moja kwa moja lakini nikawa najiuliza kwa nini sehemu tisa nilizoenda nitajiwa mtu huyo tu?
“Nikiangalia sababu, wazee hao walikuwa wananiambia kuna vitu tulikuwa tunagombania na huyo mtu, hao wazee wenyewe hawajui ni vitu gani,” alidai Tanzanite.
Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Mwandishi wetu alifanya jitihada za kumtafuta Diamond ili azungumzie madai hayo lakini hakuweza kupatikana mara moja, jitihada za kumpata zinaendelea.
Diamond na Tanzanite waliwahi kuingia kwenye bifu kisa kikiwa ni Tanzanite kugandamizia biti ya wimbo wa Mbagala katika wimbo wake Kafara.