Monday, May 13, 2013

ZIJUE SIFA ZA "MWANAUME ANAYETAKA KUWA SERIOUS NA WEWE" NA "MWANAUME ANAYEKUCHEZEA''

  ATAKAYEKUOA SIFA ZAKE NI KAMA IFUATAVYO... 1. ANABADILIKA  Mwanaume Ambaye Ana Malengo Ya Kuoa Hubadilika Kitabia. Muda Mwingi Hut... thumbnail 1 summary


 


ATAKAYEKUOA SIFA ZAKE NI KAMA IFUATAVYO...

1. ANABADILIKA

 Mwanaume Ambaye Ana Malengo Ya Kuoa Hubadilika Kitabia. Muda Mwingi Hutaka Kuonekana Mtu Mzima Mwenye Sifa Nzuri. Hatakuwa Mtu Wa Kulewa Kupita Kiasi Na Kutapanya Mali Na Wanawake Wengine. Tabia Zake Mbaya Za Zamani Ataziacha

Kisa Cha Mabadiliko Hayo Kinatajwa Na Wataalamu Wa Masuala Ya Ndoa Kuwa Ni Pamoja Na Kumshawishi Mwanamke Aliyemchagua Aitikie Mwito Wa Kuwa Pamoja Katika Maisha. Lakini Pia Ni Kuwapa Kielelezo Chema Ndungu Au Wazazi Wake Wamuunge Mkono Katika Harakati Zake Za Kuoa.

2. ATAONGEZA JITIHADA ZA KUJITEGEMEA

Mara Nyingi Wanaume Walio Makini Na Tayari Kufunga Ndoa, Wanahitaji Kuwa Na Kipato Cha Kutosha Kuweza Kuwahudumia Wake Zao Na Familia Ambazo Watakuwa Nazo Hapo Baadaye Hivyo Wanajitahidi Kutafuta Njia Za Kupandisha Hali Yao Kiuchumi.

Kama Ni Muajriwa Anaweza Akaanza Kutafuta Miradi Mingine Nje Ya Kazi Yake Ili Imsaidie Kuongeza Kipato Cha Kujikimu Na Hali Ya Maisha. Kama Alikuwa Anaishi Na Wazazi Atapanga Chumba Na Ataanza Kujitemea.

3. ANAGUNDUA KWAMBA ANAHITAJI KUITWA BABA
Njia Nyingine Ya Kugundua Mwanaume Aliye Tayari Kwa Ndoa Ni Pale Unapotembea Naye Barabarani, Anawafurahia Watoto Mnaokutana Nao Njiani Na Mara Kwa Mara Ataonekana Kukueleza Jinsi Atakavyowafanyia Watoto Wake Mara Baada Ya Kuwapata Hapo Baadaye.

Mwanaume Huyo Pia Huwa Na Tabia Ya Kufurahia Maisha Ya Ndoa Ya Watu Wengine Yaani Anapomuona Mke Na Mume Wakiwa Na Mtoto Wao Basi Hutamani Sana Mngekuwa Nyinyi. Mnapotoka Hukuita Mke Wake!

4. NI RAFIKI LAKINI NI MUME KAMILI

Mwanaume Anayetaka Kuoa Anakuwa Ni Rafiki Yako Tu Kwa Sababu Hamjafunga Ndoa, Lakini Matendo Anayokufanyia Hayana Tofauti Na Yale Ya Mtu Kwa Mkewe. Kwa Mfano Kupanga Mipango Ya Baadaye Ya Maisha Yenu, Kukutambulisha Kwa Ndugu Na Rafiki Zake. Huwa Na Hamu Ya Kutaka Kujua Matatizo Yako Na Kukusaidia Na Wakati Mwingine Kukushirikisha Katika Matatizo Yanayomkabili.

Mara Nyingi Huwa Makini Sana Kutambua Mabadiliko Ya Mapenzi Na Hutoa Uhuru Na Kukumilikisha Vitu Vyake Kwa Mfano Kukupa Funguo Za Chumba Au Nyumba Yake. Hupenda Kutoa Misaada Ya Kumwendeleza Mpenzi Wake Kimaisha, Kama Kumsomesha Au Kumtafutia Kazi.

5. HUFURAHIA UKARIBU

Mwanaume Aliyetayari Kuoa Hupenda Kuwa Karibu Na Mpenzi Wake Na Asilimia Kubwa Ya Mazungumzo Yake Atayaelekeza Katika Maisha Si Ngono. Atajitoa Kusaidia Ndugu Wa Mke Kila Linapokuja Tatizo. Na Atalalamika Anapotengwa Na Familia Ya Mchumba Wake.


SIFA ZA MWANAUME ANAYEKUCHEZEA




1. ANAKWEPA MAZUNGUMZO YA NDOA

Haonyeshi Kufurahi Unapoanzisha Mazungumzo Kuhusu Suala La Kufunga Ndoa Na Wala Hapendi Kuzungumzia Hilo. Wakati Mwingine Hata Kukutambulisha Kwa Ndugu Zake Au Rafiki Inakuwa Shida.

2. ANAGHARAMIA ANASA KULIKO MAMBO MUHIMU

Anakuwa Ni Mtu Wa Kukununulia Mapambo Ya Gharama Na Vitu Vyote Vya Anasa, Lakini Hana Mawazo Ya Kuzungumzia Maisha Yenu Ya Baadaye Wala Kukununulia Vitu Ambavyo Vitakuwa Na Manufaa Katika Maisha Ya Mbeleni. Haangalii Masuala Ya Elimu Wala Kukutafutia Mtaji Au Kazi.

3. HAJALI MACHOZI YAKO

Unaweza Kugundua Ni Jinsi Gani Hana Mpango Mzuri Na Maisha Yako, Kwani Hata Anapokuudhi Anakuwa Hajali Wala Haumizwi Na Machozi Yako, Ni Busara Kuwa Makini Kwa Sababu Huyo Atakuwa Ni Mtu Wa Kukupa Maumivu Wakati Wote.

4. HAJITOKEZI HADHARANI

Mwanaume Ambaye Malengo Yake Ni Kukuchezea Huwa Hataki Mapenzi Yenu Yajulikane Hadharani Atakuwa Mtu Wa Kutaka Mambo Yaende Kwa Siri. Hajitambulishi Kwa Rafiki Wala Kwa Ndugu Zako. Hatoi Nafasi Ya Wewe Kumtembelea Nyumbani Kwake Wala Kuwajua Wale Wa Karibu yake na familia yake.
 
Ukiona hivyo wanasema akili za kuambiwa, changanya na za kwako........
 


MAPENZI YANAPOENDA KOMBO......



Willy Anampenda Sana Lilly Lakini Anajua Fika Kwamba Mwenzi Wake Hajatulia. Hata Hivyo Anashindwa Kujipanga Kuchukua Hatua Muafaka.

Willy Anakuwa Mtu Wa Kulipuka, Akiudhiwa Na Mwenzi Wake Anatangaza Kuachana Naye Bila Kutafakari Mara Mbili...
. Haishii Hapo, Anaamka Na Chuki Mtindo Mmoja, Hata Akimkuta Barabarani Hamsalimii.

Je, Hiyo Ni Dawa? La Hasha, Kwa Kawaida Chuki Yako Itakupeleka Katika Mawazo Mengi. Utamkumbuka Kwa Mabaya Yake Lakini Hutaishia Hapo, Utaanza Kuyaona Mazuri Aliyokufanyia.
Ni Kipindi Hicho Ambacho Utaanza Kuumia Zaidi. Utatamani Yale Mazuri Yake. Inawezekana Ukakosa Aibu Na Kujikuta Wewe Mwenyewe Ndiyo Unaomba Msamaha Mrudiane.

Ukiwa Na Chuki Na Mwenzi Wako, Maana Yake Hisia Zako Bado Zipo Kwake. Akija Kuzungumza Na Wewe Ni Rahisi Kumsamehe Bila Kuzingatia Uzito Wa Kitu Alichokufanyia.
Nakusisitiza Kujua Kwamba Kinyume Cha Mapenzi Siyo Chuki. Ni Kutojali (Kupotezea). Yaani Unapokosana Na Mwenzi Wako, Usianze Bifu, Badala Yake Anza Kumpotezea Na Usimjali Kwa Chochote.

Unahitaji Kuwa Huru Na Hisia Zako. Unapoamua Kuacha Basi Simamia Uamuzi Wako. Ukizingatia Mambo Yafuatayo, Yatakupa Msaada Mkubwa Wa Kuvuka Kipindi Kigumu Cha Kuachana Na Mwenzako.

1. Mara Unapoachana Na Mwenzi Wako, Jitahidi Kadiri Uwezavyo Kuhakikisha Unasitisha Mawasiliano Naye. Iwe Kwa Simu, Ana Kwa Ana Na Mengineyo.

2. Acha Kukaribisha Hisia Kwamba Ipo Siku Wewe Na Yeye Mtarudiana. Amini Kuwa Hiyo Imetoka Jumla, Kwa Hiyo Fanya Mambo Yako, Huku Ukiamini Kwamba Mwenzi Wa Maisha Yako Anakuja.

3. Fanya Mambo Chanya Kama Vile Kujifunza Vitu Vipya, Kuongeza Ujuzi, Kufanya Kazi Kwa Bidii, Kujitolea Kwa Ajili Ya Watu Wengine, Kutoa Misaada Na Kufanya Mazoezi Ya Viungo.

Ukiyafanya Haya Yatakuwezesha Kuondoa Mawazo Hasi Kwa Mwenzi Wako Mliyeachana Na Kuzingatia Vitu Vya Msingi Ambavyo Vinahusu Ujenzi Wa Maisha Yako Ya Sasa Na Ya Baadaye.

MUHIMU:
Achana Na Hulka Za Chuki Kwa Mwenzi Wako Wa Zamani. Tangu Ulipokuwa Mdogo Mpaka Sasa Umekutana Na Marafiki Wangapi Ambao Wengine Leo Hawamo Kwenye Kumbukumbu Zako?

Mtazamo By TheDon...


UTAJUAJE KWAMBA HANA NIA NA WEWE........

ISHARA ZA MWANAUME AMBAYE HANA NIA AU HATAKI KUWA NA WEWE KATIKA MAHUSIANO YA KUDUMU (NDOA) NA WAKATI KIPINDI HICHO HICHO ANAKUTAMKIA NENO “NAKUPENDA”... Follow Me... Dr. Love...


1.HAPIGI SIMU, BALI HUTUMIA SMS

Je, Kijana Huyu Aliyekwambia Anakupenda Huwa Anawasiliana Nawe Kwa Njia Ya Ujumbe Mfupi Kuliko Anavyokupigia? Kama Utaona Hivyo, Basi Una Kila Sababu Ya Kuanza Kuitilia Shaka Nia Ya Kijana Huyu Wa Kiume, Kwani Kwa Hakika Hana Nia Yoyote Ya Dhati Ya Kuendelea Kuwa Nawe.

Kijana Wa Kiume Anapompenda Msichana, Hutamani Muda Wote Kuisikia Sauti Yake. Anapokuwa Anasisitiza Kutumika Kwa Ujumbe Mfupi Maana Yake Hana Haja Sana Ya Kusikia Sauti Yako. Naam, Ujumbe Mfupi Wa Maneno Si Njia Rahisi Sana Ya Kuwasiliana, Lakini Zaidi Ni Njia Rahisi Zaidi Ya Kuepuka Mawasiliano Na Kutoa Majibu Mafupi Kwa Mtu Ambaye Usingependa Kuwasiliana Naye.

2.HANA SABABU ZA KUCHELEWA

Unaweza Kubaini Katika Mikutano Yako Miwili-Mitatu Na Kijana Aliyekwambia Anakupenda, Kwamba Si Mtu Wa Kujali Wala Kutunza Muda. Naam, Yawezekana Katika Mara Mnazokutana, Mara Nyingi Zaidi Anachelewa Kuliko Anavyowahi. Unaweza Kudhani Kuwa Kijana Huyu Ana Mambo Mengi, Au Si Mzuri Katika Upangiliaji Wake Wa Muda, Lakini Kwa Hakika Hupaswi Kumtafutia Visingizio Hata Kama Unampenda, Kwani Kuna Uwezekano Mkubwa Kuwa Kijana Huyu Hana Mpango Na Wewe.

Kijana Wa Kiume Akikupenda Na Kupenda Kuendelea Kuwa Nawe, Lazima Tu Atakuwa Na Msukumo Wa Kutaka Kukutana Na Wewe Na Hatapenda Kukuudhi Kwa Kuchelewa. Mtu Huyu Hata Kama Atakuwa Amebanwa Vipi Kazini Ni Rahisi Sana Kutafuta Muda Wa Kukutana Na Wewe. Kinyume Chake Atakuwa Ni Mtu Wa Visingizio Vya Kuchelewa Na Wakati Mwingine Kutofika Kabisa Katika Eneo La Miadi – Hususan Kama Ameshakupata.

3.ANAWASILIANA NA MPENZI WA ZAMANI

Mwanamume Asiye Na Mpango Wa Kuendelea Kuwa Nawe Anapokuwa Amekutongoza Na Pengine Mmekutana Mara Moja Au Mbili, Atakutaarifu Kwa Kuendelea Kuwasiliana Na Mpenzi Wake Wa Zamani.

Kwa Hakika, Hakuna Jambo Ambalo Humsahaulisha Mwanamume Mpenzi Wa Zamani Kama Kumpata Mpenzi Mpya Anayempenda Kwa Dhati. Iwapo Ataendelea Kuwasiliana Na Kuzungumza Na Mpenzi Wake Wa Zamani, Hiyo Ni Ishara Kuwa Hajamalizana Na Mpenzi Wake Huyo Wa Zamani Na Pengine Bado Anatarajia Kurudiana Naye. Lakini La Muhimu Zaidi Ni Kwamba, Mwanamuke Huyu Hakupendi Kama Unavyodhani Na Wala Hajawa Tayari Kuwa Nawe Kama Mpenzi Au Mchumba.

4.HAKUTAMBULISHI KWA MARAFIKI

Mwanamume Akikupenda, Hususan Vijana Katika Zama Hizi, Lazima Tu Atakutambulisha Kwa Marafiki Zake, Maana Atakuwa Anajisikia Fahari Kwa Kufanya Hivyo, Hususan Kama Anahisi Wewe Ni Mwanamke Maridadi.

Kwa Hulka, Lazima Tu Kijana Wa Kiume Atataka Kujionesha Kwa Watu Anapokuwa Na Kimwana Maridadi Na Anayempenda Kwa Dhati. Usipoona Dalili Zozote Za Jambo Hili, Basi Chukulia Tu Kuwa Kijana Huyu Wa Kiume Hajakupenda Kama Unavyodhani.

5.HUEPUKA WATU KUWAONA PAMOJA

Mwanamume Asiye Na Mpango Wa Kuendelea Kuwa Nawe Katika Uhusiano, Hujitahidi Kuepuka Watu Kuwaona Pamoja. Ni Kweli Kuwa Si Vijana Wote Wa Kiume Wanaopenda Mapenzi Ya Maonesho Ya Kushikana Mikono Wanapotembea, Lakini Kama Ameridhika Nawe Lazima Tu Kwa Kiasi Fulani Atataka Umma Ujue.

Kwa Hakika, Kijana Wa Kiume Anapokuwa Amempenda Msichana Kwa Dhati, Hujikuta Akifanya Hata Mambo Ambayo Zamani Alikuwa Hadhani Kuwa Anaweza Kuyafanya, Ikiwa Ni Pamoja Na Kuonesha Mapenzi Hadharani, Japo Kwa Idhara Ndogo Ndogo. Kwa Tamaduni Za Magharibi Ni Kawaida Kumbusu Mpenzi Hadharani Au Kumzungushia Mkono Kiuononi, Au Kumshika Mkono, Au Kumbusu. Lakini Afrika Hata Kutoka Naye Nje Mkizungumza Huwafanya Watu Washuku Jambo. Kama Hukuliona Hilo Kwa Mpenzi Wako, Basi Chukulia Tu Kuwa Unapoteza Muda.

6.HAZUNGUMZII MIPANGO YA BAADAYE

Unapokuwa Unazungumza Na Mwanamume Ambaye Ana Mpango Wa Kuwa Nawe Katika Kipindi Chake Cha Maisha Yaliyobaki, Lazima Tu Utambaini Akiingiza Mambo Yanayohusiana Na Maisha Ya Baadaye Mkiwa Pamoja. Kwa Hakika, Utambaini Mwanamume Huyu Akitumia Nafsi Ya Kwanza Wingi Tena Katika Muda Wa Baadaye, Yaani Akizungumza Mambo Ambayo Atafanya Na Wewe Miaka Ijayo.

Iwapo Atazungumzia Klabu Fulani Aliyoiona Karibuni Lakini Akawa Hagusii Kuwa Mtakwenda Huko Siku Moja – Tena Mbaya Zaidi Akawa Anasema Kuwa Huwa Anakwenda Pale Mara Kwa Mara, Basi Tambua Kuwa Hauko Katika Mipango Yake Ya Baadaye.

7.HAKUNA MATENDO YA MAHABA

Mwanamume Asiye Na Mpango Wowote Na Wewe Si Aghalabu Kukufanyia Jambo Ambalo Utaliona La Kimapenzi Au La Kimahaba, Hususan Anapokuwa Amefanikiwa Kufanya Mapenzi Na Wewe. Ukiona Hivi, Shtuka Mapema Na Anza Kuangalia Ustaarabu Mwingine.

Haina Maana Kuwa Asipokununulia Maua Basi Hana Mpango Nawe, Lakini Angalau Mara Moja Moja Akufanyie Jambo Au Angalau Atoe Kauli Ambayo Itakusisimua Na Kukufanya Ujione Wa Thamani Na Wa Pekee Machoni Pake.

8.MIPANGO UNAPANGA WEWE

Iwapo Utabaini Kuwa Asilimia 80 Ya Mambo Mnayofanya Pamoja Unayaanzisha Wewe, Basi Una Kila Sababu Ya Kuutilia Shaka Mustakabali Wa Uhusiano Wenu.

Kama Ilivyobainishwa Awali, Mwanamume Akikupenda Atataka Muwe Pamoja Muda Mwingi, Lakini Kama Utabaini Kuwa Mipango Mingi Unaanzisha Wewe Na Unazungumza Naye Kwenye Simu Ijumaa Na Mnamaliza Bila Mwanamume Huyu Kuonesha Dalili Za Kutaka Kuwa Nawe Wikiendi, Japo Kwa Kinywaji, Basi Chukulia Kuwa Mwanamume Huyu Hana Nia Yoyote Ya Kuwa Nawe Kwa Muda Mrefu Zaidi.

9.HANA MPANGO NA WATU WAKO

Mwanamume Anayekupenda Atajishughulisha Na Mambo Yanayohusiana Na Watu Wako Wa Karibu, Hususan Ndugu, Jamaa Na Marafiki Zako. Iwpao Utabaini Kuwa Mwanamume Huyu Haulizi Swali Lolote Kuhusiana Na Familia Yako Au Marafiki Zako, Basi Tambua Kuwa Hana Mpango Wowote Wa Maana Na Wewe. Kumbuka Mwanamume Akikupenda Hujaribu Kuwafahamu Na Kuwapenda Watu Wako, Maana Amependa Boga Na Sheria Ni Kwamba Lazima Upende Na Ua Lake.

10.HAKUMBUKI LOLOTE LA MAANA

Ni Wazi Kuwa Hujakaa Sana Na Mwanamume Huyu, Lakini Angalau Kuna Mambo Muhimu Umefanya Naye Ambayo Anapaswa Kuyakumbuka. Kama Hawezi Kukumbuka Tarehe Muhimu Za Uhusiano Wenu, Mathalani Tarehe Mliyokutana Mara Ya Kwanza, Au Siku Mliyofanya Mapenzi, Basi Yamkini Mwanamume Huyu Hana Mpango Wowote Wa Dhati Wa Kuendelea Kuwa Nawe.

USIPOTEZE MUDA

Hakuna Mtu Mwenye Lengo La Kukuvunja Moyo, Lakini Ujumbe Ulio Dhahiri Ni Kwamba, Kama Unafikiria Uhusiano Wa Kudumu Na Mtu Kisha Akawa Anaonesha Ishara Zilizobainishwa Hapa, Basi Tambua Tu Kuwa Huyo Si Wako Na Atakupotezea Muda Wako Bure. Wala Usijaribu Kumlazimisha, Maana Mambo Ya Kulazimisha Huwa Hayadumu.

Ni Muhimu Sana Kuhakikisha Kuwa Mtu Unayetaka Kujenga Naye Uhusiano Wa Kudumu Anakupenda Kwa Dhati. Wala Haipendezi Kumng’ang’ania Mtu Ambaye Mapenzi Yake Kwako Ni Nusu Nusu. Hakikisha Kuwa Mtu Unayempenda Na Unayetaka Kuwa Naye Ni Yule Ambaye Amekuzimikia Na Atamani Sana Kuwa Nawe. Mtu Huyu Utampata, Hususan Kama Wewe Mwenyewe Utaweka Jitihada Za Makusudi Na Kujiweka Katika Hali Ya Kupendwa Na Kupendeka.....