[audios] Taarifa; Ikulu yakana kuhusu Rais Kikwete kuongezewa muda; TEF yamsimaisha Mulindwa uanachama
Dondoo za yaliyomo katika taarifa: Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba amevitaka vyama vya siasa, taasisi na ...
Dondoo za yaliyomo katika taarifa:
- Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba amevitaka vyama vya siasa, taasisi na asasi zilizopanga kwenda mahakamani kupinga mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya, kutimiza azma yao mara moja ili ukweli wa mambo ufahamike haraka na zoezi liweze kuendelea kwa wakati.
- Jukwaa la Wahariri Tanzania limemsimamisha uanachama kwa muda usiofahamika, mhariri wa Mtanzania Jumatano, Charles Mulindwa.
- Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu imetoa taarifa inayokana kuhusu habari zilizoripotiwa katika baadhi ya vyombo vya habari leo hii kuwa zipo njama za kutaka kumwongezea Rais Kikwete muda wa kubakia madarakani.
- Watu wawili wa jamii ya Kimasai wamefariki na wengine kuachwa wagonjwa baada ya kunywa supu ya mbuzi iliyochanganywa na miti shamba, iliyokuwa imelenga kuwapatia nguvu ya ziada ya kufanya kazi.
- Papa wa Kanisa Katoliki ameridhia ombi la Askofu Mkuu, Norbert Mtega la kustaafu katika utume wa uongozi.
- Audio ya taarifa za habari iliyosomwa kupitia TBC na kipindi cha Yaliyotukia cha WAPO FM radio
00:00
00:00
00:00
Yaliyotukia - WAPO FM Radio
00:00
00:00
00:00
Taarifa - TBC
TAARIFA YA IKULU DHIDI YA NJAMA ZA KUMWONGEZEA RAIS KIKWETE MUDA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mwenyekiti wa Chama cha CUF, Mheshimiwa Profesa Ibrahim Lipumba amekaririwa na Gazeti la Mwananchi la leo, Jumatano, Mei 15, 2013 akisema kuwa “amenasa taarifa za siri za kuwepo kwa mipango ya kuongeza muda wa Serikali ya sasa kukaa madarakani”.
Katika habari hiyo iliyoandikwa chini ya kichwa cha habari, “Lipumba: Kuna njama za kumwongezea JK muda” Mheshimiwa Lipumba anadai kuwa Serikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete “ itakaa madarakani hadi mwaka 2017” kwa sababu kuna “wasiwasi kuwa mchakato wa sasa wa kupata Katiba Mpya hautaweza kukamilika mwaka 2014.”
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, inapenda kufafanua kuwa taarifa hiyo ya Mheshimiwa Prof. Lipumba ni uzushi mtupu na ni upotoshaji usiokuwa na msingi. Rais Kikwete hafahamu kuwepo mipango hiyo. Ni vyema Mheshimiwa Lipumba aisaidie jamii kusema nani anafanya mpango huo ili ukweli ujulikane. Aidha, Mheshimiwa Rais anawasihi wanasiasa na Watanzania kwa ujumla kuacha tabia za uongo na uzushi na kuwapotezea muda Watanzania kufikiria mambo yasiyokuwepo.
Ukweli ni kwamba, kama ambavyo amesema mara nyingi, ni matarajio ya Rais Kikwete kuwa mchakato wa Katiba utakamilika mwaka 2014 na kuwezesha Uchaguzi Mkuu wa 2015 kufanyika chini ya Katiba Mpya kama inavyotarajiwa na kumpa nafasi ya kustaafu mwisho wa kipindi chake cha uongozi wa taifa letu.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
15 Mei, 2013

TAARIFA YA KUSTAAFU KWA ASKOFU MTEGA

BABA Mtakatifu Francis, amekubali ombi la Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Songea, Norbert Mtega (68),pichani, kustaafu katika utume wa kuongoza jimbo hilo.
Taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Anthony Makunde, kutoka kwa Balozi wa Papa nchini, Askofu Mkuu Frascisco Padilla, ilieleza kuwa, Papa amekubali ombi hilo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ombi la Askofu Mtega kwa Papa, lilitokana na kuwa na matatizo ya kiafya, hivyo kushindwa kuwahudumia waumini inavyopaswa. Hata hivyo, kikanisa ni siri ya mtu mwenye hadhi ya Askofu, anapoomba kwa Papa kustaafu.
“Baba Mtakatifu Francis amekubali ombi la Mhashamu Askofu Mkuu Norbert Mtega, kustaafu kutoka majukumu ya utawala wa kichungaji wa Jimbo Kuu la Songea, kwa sababu ya kiafya,” ilieleza taarifa hiyo.
Hata hivyo haikufafanuliwa maradhi yanayomsumbua Askofu Mtega, ambaye pia kiumri ni miongoni mwa maaskofu wakongwe katika kanisa hilo nchini.
Katika hatua nyingine, Papa amemteua Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa, wa Iringa, kuwa msimamizi wa kitume wakati kiti cha Askofu wa Jimbo Kuu la Songea, kikiwa wazi, kwa mamlaka ya kiti kitakatifu (Mamlaka ya Vatican).
Kwa kawaida, hakuna muda maalum wa uteuzi wa Askofu Mkuu mwingine kuongoza jimbo, panapotokea askofu amestaafu utume, lakini huchukua hata miezi sita hadi mwaka kufanyika uteuzi. Hivi sasa jimbo hilo linaongozwa moja kwa moja kutoka Vatican kwa usimamizi wa Askofu Ngalalekumtwa.
Askofu Mkuu Mtega alizaliwa katika kijiji cha Kinyika (Lupanga-Njombe), Agosti 17, 1945. Alipata daraja la Upadri Novemba 14, 1973, aliteuliwa kuwa Askofu wa Jimbo la Iringa Oktoba 28, 1985.
Aliwekwa wakfu na Papa John Paul II Januari 6, 1986, huko Roma II, na miezi miwilli baadae, Machi 9, 1986 alisimikwa Iringa. Aliteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Songea Julai 6, 1992 na kusimikwa huko Songea Septemba 20 mwaka huo huo.
Mwisho.

MEMBE (MB, W) AKUTANA NA UJUMBE WA UNAMID
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Maalum na Msuluhishi Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika katika Mgogoro wa Darfur (UNAMID), Mhe. Mohamed Ibn Chambas mara baada ya kuwasili Wizarani kwa mazungumzo. Katika mazungumzo yao walijadili masuala mbalimbali ya namna Vikosi vya UNAMID vinavyotekeleza majukumu yake huko Darfur katika kulinda Amani. Tanzania pia imechangia katika Vikosi vya UNAMID Wanajeshi wapatao 1,129. (picha: Tanzania Foreign blog)
TAARIFA YA TEF KUHUSU MULINDWA KUSIMAMISHWA UANACHAMA
Tanzania Editors Forum
AZIKIWE STREET PLOT No. 2309/50
P.O.BOX 75206 Dar es Salaam, Tanzania
Tel: +255 22 123236
Mob: +255 715 339090, +255 767 757669
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
1. Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) katika kikao chake leo, Jumatano, Mei 15, 2013 limemsimamisha uanachama kwa muda usiojulikana, Mhariri wa Mtanzania Jumatano, Charles Mulinda. Kwa maana hiyo Mulinda ataendelea kuwa nje ya TEF hadi hapo itakapoamuliwa vinginevyo.
2. TEF imechukua uamuzi huo baada ya kupokea na kujadili kwa kina taarifa ya Kamati ndogo ya wahariri watatu ambayo iliongozwa na Mhariri wa Nipashe, Jesse Kwayu kwa ajili ya kuchunguza habari iliyochapishwa na Gazeti la Mtanzania, Jumatano Aprili 17 mwaka huu ikiwa na kichwa kisemacho “Mtandao Hatari”.
3. Habari hiyo iliwataja wahariri wawili, Ansbert Ngurumo wa Tanzania Daima na Deodatus Balile wa Jamhuri kuwa ni washirika wa Joseph Ludovick, mshitakiwa katika kesi ambayo ilikuwa ikihusishwa na ugaidi (kabla ya kubadilishwa na mahakama) lakini ikiwahusisha kwa namna moja au nyingine na tukio la kuumizwa kwa Mwenyekiti wa TEF, Absalom Kibanda.
4. Yalikuwa ni maoni ya wahariri wengi katika Mkutano wa April 18, 2013, kwamba habari hiyo ilikuwa na upungufu mkubwa kitaaluma, hivyo kuamua kuchunguza habari hiyo na kubaini iwapo kulikuwa na ukiukwaji wa maadili na misingi ya kitaaluma ya habari.
5.0 Kamati hiyo pamoja na mambo mengine ilipaswa kuchunguza yafatayo:
5.1 Kuchunguza mazingira ya kuchapishwa kwa habari hiyo na kama kulikuwa na msukumo wowote nyuma ya kuandikwa kisha kuchapishwa kwakwe.
5.2 Kuchunguza chanzo/vyanzo vya habari hiyo na kubaini kama kulikuwa na ajenda maalum.
5.3 Kuchunguza ushahidi wa tuhuma zilizotolewa dhidi ya Deo Balile na Ansbert Ngurumo (kama Mullinda) alivyokiambia kikao cha Aprili 18 kwamba alikuwa na ushahidi way ale aliyoyaandika.
5.4 Kuchunguza na kubaini iwapo habari husika ilikidhi vigezo vya kitaaluma.
6.0 Katika uchunguzi wake Kamati ilibaini yafuatayo:
6.1 Kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa maadili ya kitaaluma katika mchakato mzima uliowezesha kuandikwa na kuchapwa kwa habari husika na kwamba habari hiyo haikuwa na sifa wala vigezo vya kihabari.
6.2 Mulinda akiwa Mhariri wa Gazeti la Tanzania Jumatano, alishindwa kuthibitisha usahihi wa taarifa hiyo na hata alipotakiwa kutoa ushahidi wa tuhuma dhidi ya wahariri aliowataja hakuweza kufanya hivyo.
6.3 Tangu kuandikwa kwake, kuhaririwa na hadi kuchapishwa kwa taarifa hiyo, hakukuwa na vikao rasmi vya wahariri ambavyo kimsingi ndivyo vinavyopaswa kufanya uamuzi kwamba ni habari gani ichapishwe na kwa vigezo gani.
6.4 Kwamba kulikuwa na nguvu (msukumo) ya ziada katika kuchapishwa kwa habari hiyo kwani taarifa kwamba habari hiyo ingechapishwa zilifahamika siku moja kabla ya kuchapishwa kwa habari yenyewe.
6.5 Kwamba Mhariri husika alithibitika kukaidi uamuzi wa TEF kwa kuendeleza mjadala huo katika Makala yake ya Mchokonozi ya Mei 8, 2013 iliyobeba kichwa cha Habari "Simba hapigani na Binadamu" huku akijua kuwa kufanya hivyo ni kuingilia Uhuru wa Kamati iliyokuwa ikiendelea na uchunguzi wa suala hilo.
7. 0 Hitimisho
7.1 Kwa kuzingatia matokeo hayo TEF inaushauri Uongozi wa New Habari (2006) Ltd na vyumba vingine vya habari kuboresha mfumo wake wa usimamizi wa uhariri ili kuziba mianya kwa habari tata kama hiyo ya "Mtandao Hatari" kupenya na kuwaumiza baadhi ya watu bila kuwapo kwa uthibitisho wa tuhuma husika.
7.2 TEF inaendelea kuchukua hatua nyingine za ndani kuimarisha usimamizi wa nidhamu na maadili kwa wahariri ikiwa na itaendelea kuchukua hatua dhidi ya ukiukwaji wowote ule wa kitaaluma utakaofanywa katika vyombo vya habari.
Imetolewa na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF)
Dar es Salaam, Mei 15, 2013