Monday, March 3, 2014

G7 yailaani Urusi kuihusu Ukraine

Facebook Twitter Google+ Tuma kwa rafiki yako Chapisha Maandamano ya kuipinga Urusi, Ukraine. Kundi la mataifa saba ... thumbnail 1 summary


Maandamano ya kuipinga Urusi, Ukraine.
Kundi la mataifa saba yaliyostawi zaidi kiviwanda almaarufu kama G7 limelaani vikali hatua za kijeshi zilizochukuliwa na Urusi nchini Ukraine-viongozi kundi hilo wakitaja hatua ya Urusi kama ukiukaji wa uhuru wa Ukraine.
Katika taarifa ya pamoja iliyotiwa pia saini na Umoja wa Ulaya EU-Urusi imetakiwa kushughulia wasiwasi wake kuihusu Ukraini kupitia mashauri au upatanishi.
Kundi hilo la mataifa saba tajiri zaidi duniani maarufu kama G-Seven limesema kuwa linachukuwa uamuzi wa kuahirisha matayarisho ya kongamano ambalo lingefanyika nchini Urusi mwezi juni mwaka huu kutokana na vitendo vya Moscow. Taarifa hiyo inakuja wakati vikosi vya Urusi vikiimarisha uthibiti katika rasi ya crimea ambapo Urusi inasema kuwa inalinda raia wake baada ya serikali kupinduliwa mjini Kiev.
Mbunge mashuhuri wa Urusi - Vyacheslav Nikonov, ameimabia BBC kwamba Urusi imejiandaa kwenda vitani kulinda maslahi yake nchini Ukraine na hususan katika mji wa Sevastopol.
"Ukraine ilialikwa kujiunga na Nato na hii ina maana kuwa marekani, au vituo vyake vya kijeshi vitawekwa nchini Ukraine. Urusi itafanya lolote, itahatarisha kuingia vita kuzuia hilo kutokea. Ni kuhusu kituo cha kijeshi, ni kuhusu mustakabal wa Urusi, mustakabal wa Ukraine. Sidhani kama mataifa ya magharibi yanaelewa kwamba Ukraine ni mahali ambapo Urusi ilizaliwa," amesema Nikonov.
Wanajeshi wasiotambuliwa washika doria katika kambi moja ya kijeshi nchini Ukraine.
Awali serikali ya mpito ya Ukraine iliishutumu Urusi kwa kutangaza vita na kuwaamuru wanajeshi wake kuwa tayari kwa makabiliano.Shirika la kujihami kwa mataifa ya Magharibi NATO limetowa wito kwa Urusi kuwaondoa wanajeshi wake nchini Ukrainena kuzitaka pande zote kusuluhisha mgogoro huo kwa njia ya amani. Taarifa hiyo imetolewa baada ya mkutano wa dharura wa mabalozi wa NATO mjini Brussels kujadili mgogoro huo. Katibu mkuu wa NATO, Anders Fogh Rasmussen, amesema kuwa huenda wachunguzi wa umoja wa mataifa wakatumwa kusaidia kusuluhisha hali ya mambo.
"Tunatoa wito kwa urusi kuheshimu ahadi zake za kimataifa, kuondoa vikosi vyake na kujiepusha na uvamizi katika maeneo mengine nchini Ukraine. Tunatowa wito kwa pande zote kufuata njia ya amani katika kusuluhisha mgogoro huo kupitia mazungumzo, kupitia wachunguzi wa kimataifa chini ya mwavuli wa umoja wa baraza la usalama la umoja wa mataifa au shirika la ushirikiano wa kiusalama ulaya OSCE,'' amesema bwana Rasmussen.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa marekani , John Kerry, anatarajiwa kuzuru Kiev hapo kesho jumanne kuiunga mkono serikali mpya ya Ukraine.
Haya yanajiri wakati mkuu wa jeshi la wanamaji wa Ukraine, Denis Berezovsky, akipokonywa madaraka yake baada ya kusema hadharani kwamba anaunga mkono serikali mpya ya Jimbo la Crimea ambayo inaunga mkono Urusi. Serikali ya Kiev imesema kuwa inamfanyia uchunguzi kwa nia ya kumfungulia mashtaka ya uhaini.

Oscar Pistorius akana mashitaka

Facebook Twitter Google+ Tuma kwa rafiki yako Chapisha Pistorius na marehemu menzi wake Steenkamp Mwanariadha wa Afr... thumbnail 1 summary


Pistorius na marehemu menzi wake Steenkamp
Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amekanusha mashitaka ya kumuua mpenzi wake wakati kesi yake ikianza kusikilizwa mjini Pretoria.
Pistorius ambaye ana ulemavu wa miguu na ambaye hutumia miguu bandia ameshitakiwa kwa kumuua mpenzi wake na mwanamitindo Reeva Steenkamp.
Oscar amesema alimpiga risasi marehemu kimakosa kwani alidhani alikua mwizi.
Katika siku ya kwanza ya kesi hiyo jirani wa Oscar Michelle Burger , ameambia mahakama kuwa alisikia mwanamke akipiga mayowe mapema asubuhi tarehe 14 mwezi Februari mwaka 2013.
Bwana Pistorius amekanusha madai dhidi yake kuwa alimuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Alimpiga risasi na kumuua Steenkampe aliyekuwa na umri wa miaka 29 mwanamitindo na muigizaji akisema kuwa hakumuua kwa maksudi.
Jirani ya Oscar alisema kuwa kilio cha mwanamke huyo kilifuatiwa na milio ya risasi
''alipiga nduru akitaka msaada. Pia alisikia mwanamume akipiga mayowe naye akiomba msaada, '' alisema mwanamke huyo.
Alisema punde alipopiga simu kutaka msaada kutoka kwa polisi hapo ndipo alisikia milio ya risasi.
Kukamatwa kwa Pistorius kulishangaza wengi nchini Afrika Kusini.
Pistorius mwenye umri wa miaka 27 alishinda dhahabu katika michezo ya Olimpiki ya walemavu mjini London mwaka 2012 na pia alishindana katoka michezo rasmi ya olimpiki.
Kesi hiyo ilicheleweshwa wa dakika 90 kwani mkalimani wa lugha ya Afrikaans hakuwepo mahakamani.
Pistorius inasemekana alionekana mtulivu alipowasili mahakamani.
Pistorius anasema kuwa alimpiga risasi Reeva kwa bahati mbaya akidhani alikuwa jambazi aliyekuwa amevamia nyumba yake. Mauaji yake yalitokea siku ya Valentines mwaka jana.
Wiki jana mashirika ya habari za michezo, yalipata idhini ya kupeperusha kesi ya Pistorius moja kwa moja kutoka mahakamani.

NYUMA INAUZWA

Nyumamba inauzwa location- kimara mwisho details -gari linafika hadi nyumbani            -ina vyumba vitatu ,master room na sebule ... thumbnail 1 summary

Nyumamba inauzwa
location-kimara mwisho
details-gari linafika hadi nyumbani
           -ina vyumba vitatu ,master room na sebule
           -vyumba vya nje(mabanda ya uwani) viwili(2)
           -choo cha nje na choo cha ndani na ina umeme
bei-million 48  (negotiatable)
contact:0718776676

             0653849126
e-mail:zuberiamiri@hotmail.com
           omarysaidi53@live.com




upande wa mbele inavyooneka nyumba kubwa na nyumba ndogo

                                            upande wa mbele

                                                         mbele
                                                       Ubavuni mwa nyumba
                   
                              picha ikionesha pande mbili za nyumba upande wa nyuma

                                               picha ikionesha nyumba ndogo na nyumba kubwa

 
                                               mbele        
                                
                                                  upande wa nyuma