TUNAENDELEA na mada yetu tuliyoianza wiki mbili zilizopita kuhusu namna ya kukabiliana na wivu. Endelea...
Kwa mawazo yake, tabia yako ya kutojiamini, hufikiria kwamba hakupendi.

Ikitokea akawa anafanya mawasiliano na mtu wa jinsia kama yako, hapo
unaanza kuweweseka, mara ukasirike, upekue simu yake bila sababu,
umkaripie, unune na kususa kuzungumza naye. Hiyo ni kujipa jakamoyo.
Unashindwa kujiamini kama wewe ni zaidi ya huyo anayewasiliana naye.
Unaogopa atakupora mpenzi.
Kwa mwanamke, kama anamhofia mwenzi wake…
TUNAENDELEA na mada yetu tuliyoianza wiki mbili zilizopita kuhusu namna ya kukabiliana na wivu. Endelea...
Kwa mawazo yake, tabia yako ya kutojiamini, hufikiria kwamba hakupendi.

Ikitokea
akawa anafanya mawasiliano na mtu wa jinsia kama yako, hapo unaanza
kuweweseka, mara ukasirike, upekue simu yake bila sababu, umkaripie,
unune na kususa kuzungumza naye. Hiyo ni kujipa jakamoyo. Unashindwa
kujiamini kama wewe ni zaidi ya huyo anayewasiliana naye. Unaogopa
atakupora mpenzi.
Kwa mwanamke, kama anamhofia mwenzi wake kwamba
anaweza kumsaliti kwa kutoka na mtu ambaye huwa anawasiliana naye, hiyo
ni sawa na kujiwashia taa nyekundu. Si ajabu kutokujiamini kwako
kukamfanya mwezi wako aone bora amalize kesi moja kwa moja. Vilevile,
kwa mwanamke mwenzako atavimba kichwa, kuona hujiamini kwa sababu yake.
Kwa mwanaume, itakufanya ukose sifa za kuonekana kidume. Mwenzi wako
atakuona msumbufu na unamkosea heshima kumtuhumu kwamba anaweza
kukusaliti. Amini kwamba wewe ni wa ukweli na mpenzi wako anatosheka kwa
makali ambayo unayo.
Usipojiamini, utampa kichwa huyo unayemuogopa.
Muamini kuwa hatakusaliti na endapo unadhani anaweza kukuendea kinyume,
huna haja ya kuishi naye. Ni rahisi kuonekana katuni kwenye jamii,
mjinga, bwege kama hujiamini.
Linda heshima yako, dhibiti wivu
wako, jiamini. Hayo ni mambo ambayo yanaweza kukupa uwezo wa kukabili
changamoto mbalimbali ambazo zinaweza kuusumbua moyo wako kwa kuupa
wasiwasi kuwa mwenzi wako anakuendea ndivyo sivyo.
“Yule ndugu
ananiogopa kweli, anahisi namchukua mtu wake,” hii kauli anaweza
kuitamka huyo ambaye wewe huna imani naye. Tambua kuwa unampa kichwa kwa
maana hata jinsi anavyozungumza anaashiria kuwa yeye ndiye amebeba
amani yako. Usimfanye binadamu mwenzako akajiona hivyo.
6. WASILIANA MARA KWA MARA
Una wasiwasi na mahali ambako mwenzi
wako yupo? Huna amani na unahisi anakusaliti? Moyo wako umefunikwa na
jakamoyo na kila hatua mapigo yanaongezeka kasi au yanashuka? Kimsingi
huna sababu ya kuwa hivyo. Usiishi kwa dhana, ila simamia vitu
vinavyoonekana.
Mawasiliano ni njia bora kabisa ya kudhibiti wivu.
Mnapozungumza mara kwa mara au ‘kuchati’ kwa SMS, Facebook au mitandao
mingine ya kijamii, huwaweka karibu. Kama una hali ya wasiwasi,
itakwisha au kupungua kwa sababu muda wote utajiona kama mpo pamoja.
Je, mkiwa wawili chumbani au sehemu yoyote ya faragha, bila simu wala
mtu wa tatu anayeweza kuingilia ukaribu wenu, mnaweza kuanza kulumbana
kwa sababu ya kuoneana wivu? Jibu ni hapana. Hivyo basi, mawasiliano ya
mara kwa mara huwaweka karibu na ni salama zaidi kuliko hata mngekuwa
wawili chumbani.
Mawasiliano yasiwe yenye kuishia katika simu au
mitandao, kama hamjafunga ndoa au tayari ni wanandoa lakini hamuishi
pamoja, jitahidini kukutana mara kwa mara. Ikiwa mnaishi eneo moja,
wekeni utaratibu wa kuonana kila inapobidi, hiyo itasaidia kukuza upendo
na amani ambayo itayeyusha hulka za wivu.
Wakati ukitekeleza hili
la kuonana mara kwa mara na mwenzi wako, si vibaya ukamwambia jinsi
unavyoumizwa na tabia ya yeye kufanya mawasiliano ya karibu na watu
wenye jinsia tofauti na yeye. Ukizungumza naye kwa upole, hali itakuwa
nzuri kuliko kulaumu au kulalamika.
Hoja ya wivu iwekwe mezani
halafu muijadili kwa upana. Kitendo cha kujadili na mwenzi wako jinsi
wivu unavyokutesa, kitasaidia kuweka mwanga na kupata ufumbuzi wa tatizo
husika. Kama atajua mambo ambayo akiyafanya utaumia halafu akatekeleza
bila woga, maana yake atakuwa amedhamiria kukuumiza, hivyo hakufai kwa
maisha yako.
Kama usipomwambia ukweli, itakuwa ngumu kwa mwenzi wako
kujua jinsi ya kukusaidia kuyakabili hayo maumivu unayoyapata kwa
sababu ya wivu. Waungwana wanasema kuwa dirisha la mazungumzo,
hurahisisha yabisi kuwa laini. Anza leo kuamini katika kumshirikisha
mwenzi wako uone matunda yake.
Shika kanuni hii “zungumza sana,
ubishi hapana”, utakuwa kituko endapo utajibiidisha na ubishi badala ya
kuzungumza kwa lengo la kumpa muongozo. Wivu ni chachandu lakini ukizidi
mapenzi huonekana tamu yenye uchungu.
Itaendelea wiki ijayo.