Picha ya marehemu M2 the P na Ngwair, waliyopiga usiku wa dhahama Kwa mujibu wa DJ Fetty, habari zenye uhakika zilizotoka kwa Dr aliekuw...
1:22 PM
Picha ya marehemu M2 the P na Ngwair, waliyopiga usiku wa dhahama
Kwa mujibu wa DJ Fetty, habari zenye uhakika zilizotoka kwa Dr aliekuwa ICU, katika hospitali ya St Hellen Joseph, zimethibitisha kuwa msanii aliekuwa na Ngwea wakati mauti yanamkuta, ambae yeye pia alikua hoi hospitali, anaendelea vizuri, na anaongea kwa sasa, ila uchunguzi wa kile kilichosababisha kufikishwa hospitali hapo bado unaoendelea.
M2 the P alipelekwa katika hospitali ya St. Hellen iliyopo nchini humo kwa matibabu baada ya kukutwa amepoteza fahamu akiwa na Mangwair aliyefariki dunia jana. Mwili wa marehemu Mangwair bado upo katika hospitali ya St. Hellen na mipango ya kuhamisha mwili huo bado inaendelea.
Baadhi ya Watanzania waishio nchini Afrika Kusini wamejikusanya kwa ajili ya kuandaa mipango ya kuhifadhi mwili huo pamoja na safari ya kuuleta nchini Tanzania.
Hii hapa chini ni sauti ya daktari wa hospitali hiyo akielezea hali ya msanii M2 The P, akisema hali yake imekakamaa kidogo