Monday, July 22, 2013

BABA WA KAMBO AMUUA MTOTO WA MKEWE KWA KUMOIGA NA KITU KIZITO KICHWANI HUKO TABORA..!!

  POLISI mkoani Tabora inamshikilia mkazi wa Ilolangulu wilayani Uyui, Makungu Fidel kwa tuhuma za kumuua mtoto wa mkewe m... thumbnail 1 summary

 


POLISI mkoani Tabora inamshikilia mkazi wa Ilolangulu wilayani Uyui, Makungu Fidel kwa tuhuma za kumuua mtoto wa mkewe mwenye umri wa miaka mitatu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Peter Ouma, alisema jana kwamba Fidel anatuhumiwa kumuua mtoto huyo, Kapemba Maulidi kwa kumpiga na kitu kizito kichwani.
Kwa mujibu wa Kamanda, Makungu alimuua mwanawe huyo wa kambo kwa kumpiga na kitu kizito kichwani nyumbani kwao Ilolangulu, kitongoji cha Mlimani, wilayani Uyui. Alisema chanzo cha kufanya hivyo hakijajulikana.
Kamanda alisema vitendo vya ukatili dhidi ya watoto vinaelekea vinashika kasi mkoani Tabora ingawa vingi havitolewi taarifa polisi.
Alisema wamedhamiria kutumia dawati lake la jinsia kwa ajili ya kutoa elimu kwa wazazi na walezi kuhakikisha vitendo hivyo vinakomeshwa.

CHANZO: HABARI LEO

.