Kampuni ya Nissan nchini Japani imefanikiwa kuingia kwenye headlines baada ya kufanikiwa kwa jaribio la gari walilolitengeneza ambalo linajiendesha lenyewe.
Unaambiwa limetembea umbali wa
kilometa 2.3 likijaribiwa kwenye mikikimikiki ya aina mbalimbali
barabarani kama vile kuovertake, kufata alama za barabarani, taa za
kuongozea magari na hata sehemu za watu kuvuka barabara.
Nissan wamesema wanalengo la
kuanza kuliuza hili gari miaka saba kutoka sasa, hiyo itakua mwaka 2020
ambapo gari hili lina kamera maalum pamoja na sensors
zinazofanikisha kulipa taarifa ya tukio husika kwa wakati huo ndio
maana linaweza kufanya kama inavyotakiwa mfano kushika breki, kukanyaga
mafuta na vitu vingine.
Kingine cha kushangaza, kwa
mfano kwenye miji mikubwa ambayo parking ni tatizo unaweza kuliacha
likajiendesha lenyewe kwenda kutafuta parking wakati wewe unawahi mahali
alafu ukimaliza shughuli zako unalikuta linakusubiri likiwa limepaki
vizuri kabisa.
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI
No comments
Post a Comment