30 January 2014
Aliyekuwa
Freemason kwa miaka 14 afunguliwa katika mkutano wa Ufufuo na Uzima
unaoendelea Moshi; alikatwa kidole akiwa mdogo kama udhihirisho wa alama
yao (devil horns)
alieleza mwenyewe mbele ya waliokuwepo mkutanoni maelfu ya watu wa
mkoa wa Kilimanjaro na vitongoji vyake wanaohudhuria mkutano huo katika
viwanja vya mashujaa unaoongozwa na mchungaji Josephat Gwajima wa kanisa
la Ufufuo na Uzima lenye makao makuu yake Kawe jijini Dar es salaam.
Binti
wa kiislamu ambaye aliwekwa ndani ya bahari kwa miaka mingi; alipokea
ukombozi wake mara baada ya maombezi. Kule baharini alikuwa ameolewa na
jini ambaye alimweka awe malkia wa baharini kwa miaka mingi... Mungu
akamrudisha baada ya maombezi na kumpokea Yesu Kristo.
Baadhi ya
picha jinsi maelfu ya wakazi wa mji wa Moshi mkoani Kilimanjaro
wanavyohudhuria mkutano huo toka ulipoanza tarehe 20 mwezi huu,
unatarajiwa kumalizika siku ya jumapili tarehe 27.
No comments
Post a Comment