Thursday, February 27, 2014

Viktor Yanukovych aomba Urusi kumlinda

Viktor Yanukovych anasema angali Rais wa Ukraine Baada ya kutoweka m... thumbnail 1 summary

Viktor Yanukovych anasema angali Rais wa Ukraine
Baada ya kutoweka mwishoni mwa wiki, aliyekuwa Rais wa Ukraine Viktor Yanukoovich, anasemekana kuonekana nchini Urusi.
Hii ni kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Urusi ambavyo vimenukuu taarifa kutoka kwake.
Lakini bado hakuna taarifa kamili kuhusu aliko hasa.
Katika taarifa yake alisema kuwa bado yeye ni Rais wa Ukraine ingawa anaitaka serikali ya Urusi kuhakikisha usalama wake.
Taarifa hiyo, kutoka kwa Viktor Yanukovych ilitolewa na shirika rasmi la habari la Urusi na kusomwa kwenye televisheni nchini humo
Katika taarifa hiyo amesema kuwa yungali Rais wa Ukraine na anaamini kwamba vikao vya wabunge vinavyoendelea katika bunge la Ukraine sio halali.
Alisema kuwa ameitaka Urusi kumlinda kutoka kwa watu wenye siasa kali ambao walitwa mamlaka nchini Ukraine.
Aliongeza kuwa watu wa Kusini na Mashariki ya Ukraine na katika eneo la Crimea hawatakubali hali mbaya ya kisiasa ambapo mawaziri wa serikali wanaidhinishwa na makundi ya watu na kuonya dhidi ya kutokea vita vya wenyewe kwa wenyewe katika siku zijazo.
Alikanusha madai kuwa aliamuru wanajeshi kuingilia mzozo wa kisiasa nchini humo na kuwa hatafanya hivyo kamwe ila ataendelea kutafuta suluhu.

No comments

Post a Comment