Wednesday, November 25, 2015

Wapongeza Rais Magufuli kufuta sherehe za uhuru.

Rais John Magufuli. Wananchi, wasomi, viongozi wa dini na wanasiasa wamepokea kwa hisia tofauti hatua ya Rais John Magufuli, kufut... thumbnail 1 summary

Rais John Magufuli.
Wananchi, wasomi, viongozi wa dini na wanasiasa wamepokea kwa hisia tofauti hatua ya Rais John Magufuli, kufuta sherehe za kumbumbu ya uhuru na kuifanya kuwa siku ya usafi kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu, huku wengi wakipongeza.
 
Wakizungumza na Nipashe kwa nyakati tofaut jana, walisema hatua hiyo imeonyesha jinsi Rais Magufuli alivyo na uwezo wa kufanya maamuzi kulingana na umuhimu wa jambo katika wakati husika kwa manufaa ya wengi.
Mkazi wa Tabata, wilayani Ilala, Joel Mrutu, alisema hatua hiyo kiutendaji ni jambo zuri kwani ameonyesha kukerwa na matumizi mabaya ya fedha za serikali.
 
“Hatua aliyoichukua kiutendaji ni jambo zuri kwani Rais ameonyesha anakerwa na matumizi mabaya ya fedha serikali,” alisema.
 
Alisema, Dk. Magufuli akiendelea na msimamo huo inawezekana ikapatikana Tanzania mpya wanayoitaka wananchi.
 
Mkazi wa Temeke, Ali Jabir, alisema Rais Magufuli ameonyesha mfano wa kuigwa kwa kujali maisha ya watu kwa kusisitiza fedha za umma kutumika kwenye masuala ya msingi.
 
Kwa upande wake, Bwana Afya wa Manispaa ya Kinondoni, Dk. Mathias Kapiza, alisema kitendo alichokifanya Dk. Magufuli kitasaidia kuwaamsha  kuhusu madhara na ukumbwa wa ugonjwa wa kipindupindu ulioyakumba maeneo mengi nchini na kushirikiana na serikali kupambana nao. 
 
“Mabadiliko ya kweli yameanza kuonekana kwa kufuta siku ya Uhuru na kuifanya kuwa siku ya usafi, hii itawasaidia wananchi kutambua jukumu la kupambana na maradhi na kuchukua hatua kuutokomeza,” alisema Dk. Kapiza.
 
Naye Mhadhiri wa Kikuu cha Tumaini, tawi la Dar es Salaam (Tudarco), Danford Kitwana, alisema kinachoendelea kufanywa na Rais Magufuli ni namna ya kubana matumizi  mabaya ya fedha za serikali na kupongeza siku hiyo kutumika kufanya usafi.
 
Alimtaka kuangalia sherehe nyingine ambazo hazina umuhimu wa kutumia fedha nyingi ili fedha hizo zielekezwa kwenye mambo yenye tija kitaifa. Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli Kanda ya Dar es Salaam, Yasin Mleke, alisema anaunga mkono hatua hiyo kwani hali ya uchumi ni mbaya huku serikali ikiwa ina mambo mengi ya kufanya ikiwamo malipo ya mishahara  ya watumishi, madeni ya wafanyakazi, uboreshaji wa huduma za afya na elimu.
 
Naye Msemaji wa Jumuiya za Taasisi za Kiislamu Tanzania ambaye pia ni Katibu wa jumuiya hiyo, Sheikh Rajab Katimba, alisema hadhani kama ni sahihi kufuta sherehe hizo kwa kigezo cha kuifanya siku ya usafi ndiyo nchi nzima itakuwa safi.
 
Alisema kufanya hivyo  kunapoteza historia ya nchi na kutaka suala la usafi kuwekewa mikatati na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
 
Aliyekuwa Mgombea ubunge Jimbo la Segerea, Julius Mtatiro, alisema yeye haamini katika matamko badala yake vitu vinavyofanyika kisheria na siyo mtu kufanya kwa ajili ya utawala wake.
 
Alisema sherehe za Uhuru zinatakiwa kuwapo kila mkoa pasipokuwapo mambo mengi yatayogharimu fedha, ikiwamo kurusha ndege za kivita hewani, magwaride na maonyesho ya makomando na posho.
 
Mtatiro alisema huenda hatua hiyo imefanyika kutokana Hazina kuishiwa fedha, akidai kuwa nchi nyingi za Afrika vyama tawala hutumia fedha za serikali kwenye uchaguzi.
 
Ijumaa iliyopita Rais Magufuli alizuia matumizi y Sh. milioni 265 zilizokusudiwa kutumiwa na Ofisi ya Bunge kwa ajili ya hafla ya wabunge kupongezana baada ya uzinduzi rasmi wa Bunge la 11, mjini Dodoma.
 
Aliamuru zitumike Sh. milioni 15 tu na fedha nyingine zilizobaki  zitumiwe kununua vitanda kwa wagonjwa wanaolala chini katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
 
Aidha, Jumatatu iliyopita aliagiza kufutwa kwa sherehe za Uhuru na kutaka siku hiyo itumike kufanya usafi nchi nzima.
CHANZO: NIPASHE

Magufuli kufyeka nusu ya Wizara za Kikwete.

Mpango wake ni kuteuwa idadi ndogo ya mawaziri ambao ni wachapa kazi kama ilivyokuwa katika enzi ya awamu ya kwanza ya hayati baba wa ... thumbnail 1 summary

Mpango wake ni kuteuwa idadi ndogo ya mawaziri ambao ni wachapa kazi kama ilivyokuwa katika enzi ya awamu ya kwanza ya hayati baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, anatarajiwa kuzifuta wizara 15 kati ya zilizopo sasa na kubaki na baraza dogo litakalokuwa na wachapakazi makini ili kutimiza dhamira yake ya kubana matumizi na kuinua maisha ya Watanzania.
 
Kadhalika, inaelezwa kuwa Dk. Magufuli aliyeahidi kuleta mabadiliko ya kweli wakati akiomba kura kwa Watanzania kabla ya kuibuka na ushindi wa asilimia 58.46 dhidi ya wapinzani wake katika uchaguzi mkuu Oktoba 25, sasa yuko mbioni kutangaza baraza lake la mawaziri litakalokuwa na wizara 15, idadi inayofanana kwa kiasi kikubwa na ile ya Baraza la Mawaziri la miaka ya 1980 lililoundwa na Rais wa Awamu ya Kwanza, Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere. Serikali ya awamu ya nne ya Rais Jakaya Kikwete, ilimaliza muda wake Novemba 5, 2015  ikiwa na Wizara 30. Kadhalika, alipoingia kwa mara ya kwanza mwaka 2005, Rais Kikwete alikuwa na serikali kubwa yenye mawaziri na naibu wao zaidi ya 60.   
 
Kufikia leo, Rais Magufuli aliyeapishwa Novemba 5, mwaka 2015, tayari ameshamteua Mbunge wa Ruangwa, Kassim Majaliwa, kuwa Waziri Mkuu wa serikali yake ya awamu ya tano na Ijumaa iliyopita alizindua rasmi Bunge la 11.
 
Chanzo kimoja cha uhakika kimeiambia Nipashe jana kuwa hivi sasa, tayari Rais Magufuli kwa kushirikiana na wasaidizi wake, ameshakamilisha sehemu kubwa ya mchakato wa kuunda baraza lake la mawaziri na kwamba, kinachosubiriwa sasa ni kulitangaza wakati wowote kuanzia sasa.
 
Chanzo hicho kiliambia Nipashe kuwa Dk. Magufuli ambaye amejichimbia mjini Dodoma tangu mwishoni mwa wiki iliyopita, anatarajiwa kutangaza baraza lake dogo la mawaziri wakati wowote kuanzia leo.
 
“Halitakuwa sawa na hili alilomaliza nalo Rais Kikwete… na wala halitakuwa na watu wengi kama lile aliloingia nalo kwa mara ya kwanza Rais Kikwete mwaka 2005. Ni baraza dogo tu na wizara kadhaa hazitakuwapo,” chanzo kiliiambia Nipashe.
 
Kwa mujibu wa ibara ya 55 (1) ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mawaziri wanakuwa wajumbe wa Baraza la Mawaziri na pia kwa mujibu wa ibara ya 54, mawaziri huteuliwa na rais baada ya kushauriana na Waziri Mkuu. 
 
 “Kuna mambo madogo bado hayajakamilika… baada ya hapo Mheshimiwa Rais atalitangaza Baraza la Mawaziri siku yoyote kuanzia leo. Kimsingi mkakati wake ni kuwa na baraza dogo lenye wizara 15,” kilieleza chanzo hicho.
 
Aidha, ilielezwa zaidi kuwa sura kadhaa katika baraza hilo dogo zitakuwa mpya na kwamba, mawaziri waliokuwamo katika serikali ya awamu ya nne wana nafasi ndogo ya kuteuliwa katika baraza hilo.
 
“Kwa kiasi fulani Baraza hili jipya linafanana na lile la Serikali ya Mwalimu Nyerere miaka ya 1980… lina wizara chache sana, zenye lengo la kubana matumizi ya serikali lakini likiwa na uhakika wa kuchapa kazi usiku na mchana ili kutimiza lengo la Rais Magufuli katika kuwaletea maisha bora Watanzania,” chanzo kiliongeza.
 
BARAZA LA MAWAZIRI LA NYERERE
Uchunguzi wa Nipashe kupitia vyanzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na maandiko mbalimbali, umebaini kuwa iwapo Magufuli ataunda Baraza lake kwa kuangalia muundo wa Mwalimu Nyerere miaka ya 1980, maana yake baadhi ya wizara maarufu hazitakuwapo tena kwani zitakuwa miongoni mwa zile 15 zitakazofutwa na majukumu yake kuhamishiwa katika wizara nyingine za idadi kama hiyo zitakazosalimika.
 
Kumbukumbu zinaonyesha kuwa miaka ya 1980, Mwalimu Nyerere alikuwa na serikali yenye wizara 15; ambazo ni Wizara ya Elimu; Wizara ya Mipango; Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa; Wizara ya Mambo ya Ndani; Wizara ya Ujenzi; Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi na Wizara ya Kazi na Ustawi wa Jamii.
 
WQizara nyingine wakati huo ni Wizara ya Habari na Utamaduni; Wizara ya Afya; Wizara ya Nishati, Madini na Maji; Wizara ya Sheria;  Wizara ya Viwanda na Biashara; Wizara ya Kilimo na Wizara ya Fedha.
 
KASI YA MAGUFULI
Wakati Watanzania wakiendelea kusubiri kwa hamu kusikia baraza la mawaziri la Rais Magufuli, inaelezwa kuwa baadhi ya wabunge kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) wako njiapanda kuhusiana na majina ya wateule watakaokuwamo katika kuunda serikali. 
 
Inaelezwa kuwa, kama ilivyokuwa katika uteuzi wa jina la Waziri Mkuu, hivi sasa kuna usiri mkubwa pia kuhusiana na majina ya wateule wa Rais Magufuli kwa nafasi hizo za uwaziri.
 
“Tofauti na ilivyokuwa katika mika michache ya hivi karibuni, uteuzi huu wa mawaziri umebaki kuwa wa siri sana na hadi sasa hakuna majina ya uhakika ya watu wanaotazamiwa kuwamo kwenye Baraza la Rais Magufuli, “ mmoja wa wabunge aliiambia Nipashe jana.
 
Ilielezwa zaidi kuwa mbali na kuwapo kwa usiri mkubwa, pia staili ya utendaji kazi aliyoanza nayo Rais Magufuli imekuwa ikiwatisha baadhi ya wabunge wa CCM waliokuwa na matumaini ya kuteuliwa kuwa mawaziri.
 
“Misimamo ya Rais Magufuli haitoi matumaini ya ulaji kwa wateule wa nafasi hizo… wengine wameshaanza kuingiwa hofu kwamba hata wakiteuliwa, hakuna maslahi makubwa binafsi watakayoyapata zaidi ya kutakiwa wajiandae kutumikia wananchi kwa moyo mmoja na tena kwa kujituma kwelikweli, chini ya Magufuli uwaziri siyo kazi rahisi ya kuikimbilia,” mbunge mwingine aliongeza.
 
Katika hotuba yake Ijumaa wakati akizindua Bunge, Rais Magufuli alianisha mambo kadhaa aliyosema yamekuwa kero kubwa kwa wananchi na hivyo serikali yake itafanya kazi kubwa ya kuyashughulikia, baadhi ya maeneo hayo yakiwa ni ya kuboresha elimu ambayo itatolewa bure hadi kidato cha nne, kuinua mapato na pia kupambana na kukomesha vitendo vya rushwa na ufisadi.
 
Kadhalika, hivi karibuni Rais Magufuli ametangaza hatua kadhaa za serikali yake kubana matumizi na badala yake kuelekeza fedha katika shughuli za maendeleo; baadhi ya hatua hizo zikiwa ni kupiga marufuku safari holela za viongozi kwenda nje ya nchi, kufuta sherehe siku ya uhuru na badala yake kuamuru siku hiyo iwe ya kufanya usafi ili kukabiliana na kipindupindu na pia aliamuru zaidi ya Sh. milioni 200 zilizochangwa kwa ajili ya wabunge kupongezana baada ya kuapishwa wiki iliyopita zielekezwe katika Hospitali ya Muhimbili ambako zilisaidia kununuliwa kwa vitanda vya wagonjwa 300. 
 
 “Tusubiri tu kusikia baraza lake la mawaziri limewajumuisha kina nani. Lakini ukweli unabaki palepale kwamba uwaziri siyo kazi lelemama kwa serikali hii. Maana Rais (Magufuli) kaweka wazi kuwa mtu (Waziri) yeyote akiboronga, anamfuta kazi mara moja…  kinachotakiwa ni kazi tu, hakuna kwenda Ulaya ovyo, wala hakuna tafrija na makongamano yenye nia ya kuhalalisha ulaji kwa vigogo,” chanzo kiliongeza.
 
CHANZO: NIPASHE

Kigogo mmoja wa CCM amnajisi mtoto wake

Kigogo mmoja wa CCM wilayani Rombo anadaiwa kumnajisi mtoto wake mwenye umri wa mwaka mmoja. --->Mama mzazi wa mtoto huyo alidai kuwa ... thumbnail 1 summary
Kigogo mmoja wa CCM wilayani Rombo anadaiwa kumnajisi mtoto wake mwenye umri wa mwaka mmoja.
--->Mama mzazi wa mtoto huyo alidai kuwa tukio hilo lilitokea Novemba 17, usiku nyumbani kwao Mwanga walipokuwa wamelala na alishtuka baada ya kusikia sauti ya mtoto akilia kutokea chumba kingine