Thursday, June 13, 2013

MJUE MAREHEMU LANGA KILEO 'LANGA'

Ni mtaalamu na mwanamuziki stadi wa Hip Hop nchini aliyeweka wazi kuathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya.  Ili kuonyesha ... thumbnail 1 summary


Ni mtaalamu na mwanamuziki stadi wa Hip Hop nchini aliyeweka wazi kuathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya.

 Ili kuonyesha anachukizwa, Langa alilieleza jarida moja la burudani kwamba anakusudia kuanzisha Taasisi ya kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya.

Alisema matumizi ya dawa hizo yaliathiri shughuli zake za muziki na hakuwa na jambo lolote endelevu katika muziki wake.

Kimuziki Langa alianzia kundi la Wakilisha akiwa na Witness Mwaijega na Sarah Kaisi, ambapo walikuwa washiriki wa mashindano ya muziki ya Cocacola Pop stars, yaliyofanyika nchini Afrika Kusini.

Wakiwa na kundi hilo walifanikiwa kufyatua kibao cha ‘Hoi’, ambacho kiliteka wapenzi wa muziki.

Baadaye Sarah Kaisi (Shaa) alijitoa. Lakini Langa na Witness walifyatua kibao cha ‘No Chorus’.

Baada ya hapo Langa alifyatua kibao chake cha kwanza akiwa mwanamuziki binafsi, ‘Matawi ya Juu’ ambacho Dj John Dilinga (JD) aliwahi kuelezea ni moja ya kazi nzuri kutoka kwake, licha ya dosari za matumizi ya lugha.

Hata hivyo Langa alionyesha yeye ni bora na ana kipaji cha muziki. Amekuwa shujaa kwa kuendesha kampeni kali za kupinga matumizi ya dawa za kulevya kwa vijana. Serikali inapaswa kusaidia juhudi zake pamoja.

Huyu ni mmoja wa matunda ya shindano la muziki la Coca-Cola Pop Stars mwaka 2004 ambalo washindi wake waliounda kundi la Wakilisha.  Mbali ya Langa, wengine ni Sarah Kaisi `Shaa’ na Witness Mwaijaga `Witness’. Huo ndio uliokuwa mwanzo wa kung’ara kisanii kwa wakali hao, ingawa kwa sasa kundi hilo limesambaratika, kila mmoja akitamba kivyake. 

Lakini kwa bahati mbaya, mmoja wao, Langa kwa miaka ya hivi karibuni hakusikika kabisa, jambo lililomlazimu mwandishi wa makala haya kumtafuta sababu za ukimya wake.


Haikuwa kazi rahisi, lakini hatimaye Langa alipatikana na bila kutafuna maneno alisema kwamba, alishindwa kufanya kazi baada ya kuwa `teja’ aliyekubuhu.

Yaani alizama katika matumizi ya dawa za kulevya kiasi cha kupoteza kabisa mwelekeo si wa kisanii pekee, bali hata kimaisha.

“Siyo siri, kilichokuwa kimenifikisha katika hali hiyo ni dawa za kulevya. Kwa miaka mitano nilitumia sana Cocaine, Heroin, bangi na pombe. Namshukuru Mungu sasa nimerejea katika hali yangu.

“Siamini kama nimenusurika kwa sababu madawa yalinitesa, nikafanya mengi ya ajabu yaliyoichukiza familia yangu na marafiki ikiwa pamoja na kuwa mwizi na mkabaji mitaani na nyakati za usiku,” anasema Langa ambaye kundi lao la Wakilisha lilitamba na nyimbo kama `Unaniacha Hoi’ na `Kiswanglish’.

Anaeleza kwamba, kwake hayo ndiyo aliyoyaona maisha yanayomfaa, akidai awali alikuwa amechoshwa kuishi kwa masharti kutoka kwa wazazi wake waliokuwa wanampa mwongozo wa maisha, lakini bila kujua akadhani `anachungwa’. 

Kwamba, umaarufu na ngekewa ya kuzishika pesa katika umri mdogo kupitia muziki vilimtia kiburi zaidi, na hivyo kuamua kujitenga kabisa na familia yake iliyomlea kwa mapenzi mazito.

“Niliamini naweza kujitegemea kupitia kazi yangu ya muziki, nikajichanganya mtaani,” anasema kijana huyo aliyetoa kibao chake cha kwanza, Matawi ya Juu mara baada ya kusambaratika kwa kundi la Wakilisha kutokana na kila mmoja kuamua kujitegemea kimuziki. Na kweli, Matawi ya Juu ilidhihirisha kuwa Langa ni moto wa kuotea mbali katika fani. Aliweza kusimama kwa miguu yake na kutikisa.

Mwenyewe anasema: “Jina hilo la Matawi ya Juu lilidhihirisha hivyo pale video ya kibao hicho ilipotajwa kuwania Tuzo za MTV Base kwa upande wa hapa Bongo miaka michache iliyopita, kisha kutwaa Tuzo ya Kisima nchini Kenya.

“Moto huo uliwafanya baadhi ya wasanii wakongwe katika gemu ya Bongo Fleva kunitafuta na kunipa majukumu ya kushiriki katika kazi zao, ikiwemo Chagua Moja ya Farid Kubanda `Fid Q’. 

“Baada ya kuona wakongwe wamekubali vitu vyangu na kuanza kunishirikisha…nikapata pia safari za nje ya nchi. Huko Nairobi (Kenya) niliweza kufanya kazi na vichwa vikali vinavyounda Kundi la Necessary Noise, Naaziz na Wyre (Kevin Wyre).

Anasema mafanikio hayo yalimtuma kufyatua albamu yake ya kwanza aliyoipa jina la Langa, akiamini itampaisha zaidi kimaisha na kimuziki. Hata hivyo, mambo yalikwenda kinyume. Anasema alipoipeleka sokoni, wauzaji wakubwa waliigomea, hivyo kumpa wakati mgumu wa kuwaza na hatimaye kujikuta akiongeza kasi ya matumizi ya dawa za kulevya.

Siyo siri, kugoma kwa albamu yangu sokoni kulichangia kasi ya kutumia dawa za kulevya…niliona ni njia pekee ya kuondoa mawazo kwa sababu kazi iligoma, na home (nyumbani) nilishaharibu.

Sikufanya tena kazi kwa umakini na kila kazi niliyoitia haikufanya vizuri….” Anasema kwamba, baada ya mambo kumwendea mrama, ndipo alipoanza kuiba vitu nyumbani kwao kwa lengo la kuviuza na inapotokea amekosa, alidiriki hata kupiga debe katika vituo vya mabasi ili mradi apate fedha za kununua `unga’. 

Haikuishia hapo, kwani anasema alijiingiza katika kundi la wahuni waliojihusisha na wizi na ujambazi. “Kwa ujumla nilipoteza mwelekeo. Maisha yangu yakawa ya kutembea na kisu kama kitendea kazi changu katika wizi,” anasema huku akitikisa kichwa kama ishara ya kujutia matendo aliyoyafanya kwa msukumo wa madawa ya kulevya. Anakumbuka akiwa mtumwa wa `unga’, aliingia katika mikasa kadhaa ikiwa pamoja na kupigana na polisi baada ya kunaswa na dawa hizo haramu. 

Katika wizi, chochote alichokikuta mbele yake kilikuwa halali. Anasema alikwapua vitu magengeni, madukani na hata magari yaliyoegesha vibaya alinyofoa vioo na mashine zinazosaidia kupandisha na kushusha vioo ndani ya gari. 

“Ni matukio ya aibu. Yanasikitisha…,” anasema Langa anayedokeza kwamba, akiwa mtumiaji wa `unga’, alikuwa anakutana na wasanii na watu wengine mashuhuri. Hata hivyo anakataa kuwataja, akidai ni siri yake. `Ufufuo’ wa Langa kutoka katika lindi la mateso ya dawa za kulevya ulipatikana kuanzia Machi mwaka huu, baada ya familia yake kumpeleka kijana wao kwa tiba maalumu ya kuachana na matumizi ya `madudu’ hayo. Na kweli, elimu imemwingia na kujikuta akirejea ufahamu wake wa kawaida.

Ametangaza kuachana na `unga’, pombe, sigara na badala yake amejikita zaidi katika mazoezi ya kurudisha mwili wake katika hali ya kawaida. Aidha, amekata shauri la kuirudia fani yake na tayari ana vitu vipya, Bombokiata na Mteja Aliyepata Nafuu.

Anasisitiza kwamba, kutokana na mateso aliyoyapata, anakusudia katika siku za baadaye afungue kituo chake cha tiba ya dawa za kulevya ili aweze kuwaokoa vijana wengine wanaoangamia kutokana na matumizi ya dawa hizo haramu zinazopigwa vita karibu kote duniani. “Nimenusurika, namshukuru Mungu.

Nami najipanga kutaka kuwasaidia wengine waachane na mateso ya dawa za kulevya. Pia nichukue fursa hii kuwaomba msamaha wote niliowakosea kwa namna moja ama nyingine wakati nikiwa `teja’,” anasema Langa, kijana mwenye umri wa miaka 25.

Je, historia ya maisha ya Langa ikoje? Anasema Desemba mwaka 1985 jijini Dar es Salaam akiwa tunda la wanandoa Vanessa Kimei na mumewe Mengisen Kileo. Alisoma Shule ya Msingi Olympio na Sekondari ya Loyola, zote za jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, akiwa kidato cha pili alihamishiwa Kampala, Uganda katika Shule ya Vienna na baadaye Shule ya Hillside International Academy, huko huko Uganda. Baadaye alirejea nchini na kujiunga na masomo ya Stashahada ya Masoko katika Chuo cha Biashara Dar es Salaam (CBE), Kampasi ya Dodoma.

Huyo ndiye Langa Kileo msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye baada ya kulewa umaarufu na kujikita katika matumizi ya dawa za kulevya, ameibuka na kujutia `ujanja pori’, sasa akitaka kujiingiza katika kampeni ya kuwaokoa vijana wengine waliozama katika `unga’. Anakusudia pia kurudi darasani kujiendeleza na masomo ya elimu ya juu. Je, atafanikiwa? Kwa hakika, hili ni jambo la kusubiri na kuona.

Tuesday, June 11, 2013

Muigizaji wa filamu nchini, Jaji Khamis (Kashi) afariki dunia leo mchana

Msanii wa filamu nchini Jaji Khamis (Kashi) aliyewahi kutamba na michezo ya ITV enzi zile akiwa na wasanii kama mzee Masinde, Samson na... thumbnail 1 summary

kash-jaji-khamis
Msanii wa filamu nchini Jaji Khamis (Kashi) aliyewahi kutamba na michezo ya ITV enzi zile akiwa na wasanii kama mzee Masinde, Samson na wengine katika mchezo wa Tamu chungu na mingine mingi Amefariki dunia mchana huu katika hosptali ya taifa ya muhimbili alikokuwa amelazwa.

Taarifa za awali zinasema kuwa alikuwa amelazwa hapo kwa muda kiasi kabla ya kufikwa na mauti hayo.

Kwa mujibu wa matandao wa Bongo5, muigizaji mwenzie, Monalisa amethibitisha kifo cha Kashi. Aliongeza kuwa alipata taarifa kwamba Kashi amelazwa Muhimbili akiwa amezidiwa kiasi ha kushindwa kuongea. Monalisa amesema hajajua ni nini kilikua kinamsumbua marehemu Kashi. Msanii Hemedi PHD naye ame-tweet kuhusu taarifa za msiba huo.

Sunday, June 9, 2013

Kala Jeremiah, Ommy Dimpoz, Diamond & Chalz Baba watesa KTMA. List ya washindi wote

Ommy Dimpoz akichukua tuzo ya Video Bora ya Mwaka kwa music vide ya wimbo wa “Baadae” Ben Pol alipochukua tuzo ya Mtunzi Bora wa Mash... thumbnail 1 summary



Ommy Dimpoz akichukua tuzo ya Video Bora ya Mwaka kwa music vide ya wimbo wa "Baadae" Ommy Dimpoz akichukua tuzo ya Video Bora ya Mwaka kwa music vide ya wimbo wa “Baadae”
Ben Pol alipochukua tuzo ya Mtunzi Bora wa Mashahiri Bongo Fleva. Ben Pol alipochukua tuzo ya Mtunzi Bora wa Mashahiri Bongo Fleva.
Msanii wa Bongo Flava kutoka Mwanza, Kala Jeremiah aliibuka na tuzo tatu za Kili Music Awards (KTMA 2013) zilizofanyika jana usiku.  Kala alishinda tuzo ya wimbo bora wa mwaka  (Dear God) na pia aliibuka na tuzo ya msanii bora wa Hip Hop kwa kuwabwaga Fid Q, Joh Makini, Profesa Jay na Stamina waliokua pia nominees kwenye tuzo hiyo.
Advertisement
Ommy Dimpoz naye alishinda  tuzo tatu. Ommy alitwaa tuzo mbili kwa kupitia nyimbo ya “Me and You” aliyofanya collabo na Vanessa Mdee; wimbo bora wa Bongo Pop,  na wimbo bora wa kushirikiana/Kushirikishwa. Ommy alichukua tuzo ya tatu ya video bora ya mwaka kwa kupitia nyimbo ya “Baadae.”
Msanii Diamond Platnumz, ambaye hakuhudhuria tuzo hizo, alishinda moja ya tuzo kubwa usiku huo ya msanii bora wa kiume kwa kuwabwaga Ben Pol, Linex, Mzee Yusuf na Ommy Dimpoz ,na pia alishinda tuzo ya Msanii bora wa kiume Bongo Flava.
Tuzo za muziki wa dance zilitawaliwa na Chalz Baba wa Mashujaa Band aliyeibuka tuzo mbili za Msanii bora wa kiume Bendi na Mtunzi bora wa mashairi – Bendi.
Ifuatayo ni list kamili ya tuzo hizo.
Wimbo bora wa mwaka
Dear God – Kala Jeremiah
Msanii bora wa Kiume
Diamond
Msanii bora wa kike
Lady Jaydee
Msanii bora wa kike Taarab
Isha Mashauzi
Msanii bora wa kiume Taarab
Mzee Yusuf
Msanii bora wa kiume Bongo Flava
Diamond
Msanii bora wa kike Bongo Flava
Recho
Msanii bora wa Hip Hop
Kala Jeremiah
Msanii bora wa kiume Bendi
Chalz Baba
Msanii bora wa kike Bendi
Luiza Mbutu
Msanii bora anayechipukia
Ally Nipishe
Video bora ya mwaka
Baadaye – Ommy Dimpoz
Mtunzi bora wa mashairi Taarab
Mzee Yusuf
Mtunzi bora wa mashairi Bongo Flava
Ben Pol
Mtunzi bora wa mashairi hip hop
Kala Jeremiah
Mtunzi bora wa mashairi Bendi
Chalz Baba
Mtayarishaji bora wa mashairi muziki wa kizazi kipya
Man Walter
Mtayarishaji wa wimbo wa mwaka – Taarab
Enrico
Mtayarishaji wa wimbo mwaka – Bendi
Amoroso
Mtayarishaji chipukizi wa mwaka
Mesen Selekta
Rapper bora wa bendi
Fagasoni
Wimbo bora wenye vionjo vya asili
Chocheeni Kuni – Mrisho Mpoto ft Ditto
Wimbo bora wa bendi
Risasi Kidole – Mashujaa Band
Wimbo bora wa Reggae
Kilimanjaro – Warriors from The East
Wimbo bora wa Afrika Mashariki
Valu Valu – Jose Chameleone
Wimbo bora wa Bongo Pop
Me an You – Ommy Dimpoz ft Vanessa Mdee
Wimbo bora wa kushirikiana/Kushirikishwa
Me and You – Ommy Dimpoz ft Vanessa Mdee
Wimbo bora wa Hip Hop
Nasema Nao – Nay wa Mitego
Wimbo bora wa rnb
Kuwa na Subira – Rama Dee ft. Mapacha
Wimbo bora wa ragga/ dancehall
Predator – Dabo
Wimbo bora wa Taarab
Mjini Chuo Kikuu – Khadija Kopa
Wimbo bora wa zouk rhumba
Ni wewe – Amini
Bendi bora ya mwaka
Mashujaa Band
Kikundi bora cha Taarab
Jahazi Modern Taarab
Kikundi bora cha muziki wa Kizazi kipya
Jambo Squad
Hall of Fame – Institution
Kilimanjaro Band wana Njenje
Hall of Fame – Individual
Salum Abdallah

Saturday, June 8, 2013

HAYA NDIO MAMBO MAKUU 5 YA KUSHANGAZA WAKATI WA MAZISHI YA NGWEA..!!

    HUKU Albert Kenneth Mangwea ‘Ngwea’ akiwa kaburini siku ya pili leo kufuatia kufariki dunia ghafla usingizini nchini A... thumbnail 1 summary



  
HUKU Albert Kenneth Mangwea ‘Ngwea’ akiwa kaburini siku ya pili leo kufuatia kufariki dunia ghafla usingizini nchini Afrika Kusini, Mei 28, mwaka huu, mambo matano ya kushangaza yamezuka katika kipindi chote cha msiba, Risasi Jumamosi linakupa kila kitu.
Kwa mujibu wa utafiti wetu wa kina, waombolezaji mbalimbali wamekuwa wakiyazungumzia mambo hayo huku wengine wakihoji kuwepo kwake.
1. RIPOTI YAFICHWA KIBINDONI
Usiku wa kuamkia mazishi yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kihonda, Morogoro, paparazi wetu alipata bahati ya kuzungumza na mama wa marehemu Ngwea, Denisia Mangweha.
Katika mazungumzo hayo, mwanahabari wetu alimuuliza mama huyo kama alikuwa amekabidhiwa ripoti ya daktari inayotatua fumbo la nini kilimuua Ngwea.
Haya hapa majibu ya mama huyo:
“Sijapata wala sijui chochote kuhusu hiyo ripoti, wala sijui nani anayo.”
Jumanne iliyopita, ilidaiwa kuwa Mtangazaji wa Clouds FM, Millard Ayo aliyekuwa ‘Sauzi’ ndiye aliyekabidhiwa ripoti hiyo ambapo na yeye aliikabidhi kwa ndugu wa marehemu.
Kwa kawaida, ripoti inayoweka wazi kiini cha kifo cha marehemu husomwa siku ya mazishi, jambo ambalo halikufanyika siku ya kumzika Ngwea.
MANENO YA WATU MAKABURINI
Baadhi ya waombolezaji waliokuwa makaburini hapo, walitoa hisia zao wakidai kwamba, inawezekana ripoti hiyo haikuwa nzuri hivyo ili kulinda heshima ya marehemu ililazimika kuiacha kibindoni.
2. MAMA WA MAREHEMU AMTAMBUA DEMU MZUNGU
Jumatano, siku moja kabla ya mazishi, mama wa marehemu alimshika mkono aliyekuwa mchumba wa marehemu, yule mwanamke Mzungu akisema Albert (Ngwea) alikuwa akienda naye nyumbani hapo (Morogoro).
Alisema mara kadhaa walitoka yeye, marehemu na Mzungu huyo kwenda kula ‘bata’ mahali kabla ya kurejea Dar. Kwa hiyo Mzungu ni mwanamke aliyekuwa akitambulika na mama wa marehemu.
Cha kushangaza, dada wa marehemu aitwaye Neema Mangweha, alisema mchumba wa marehemu anayemjua yeye anaitwa Siwema ambaye kwa sasa ana ujauzito wa mwanamuziki maarufu wa muziki wa kizazi kipya Bongo.
 

3. MTOTO WA MAREHEMU AIBUKIA MAKABURINI
Alhamisi, wakati msafara wenye mwili wa marehemu ukiwa makaburini, mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Paulina Jeremiah akiwa na mtoto wa kike alijitokeza hadharani na kukutana uso kwa uso na paparazi wetu akidai mtoto huyo ni wa marehemu Ngwea.
Mwanamke huyo, mkazi wa Kigamboni, Dodoma alisema mtoto huyo anaitwa Neema Albert, alimzaa mwaka 2001 wakati huo Ngwea alikuwa akisoma Sekondari ya Mazengo.
Wakati anajieleza hayo, ndugu wawili wa marehemu walitokea, mmoja akiitwa Anthony Kenneth Mangweha na kumsikiliza mama Neema.
Anthony alimuuliza mama Neema kama kuna ndugu yeyote wa marehemu anayetambua uwepo wa mtoto huyo, mama Neema akawataja.
Aliwataja vijana watatu kwa jina mojamoja, Frank, Jotam na Amani ambapo alisema waliwahi kutumwa na marehemu kwenda Dodoma kumwangalia mtoto huyo.
Anthony alikiri kuwa vijana hao watatu ni ndugu wa familia hiyo na akamtaka mama Neema kupoa, baada ya mazishi na kurudi nyumbani watakaa kuzungumzia suala hilo.
4. M 2 THE P AIBUKIA KWENYE KUAGA MWILI
Katika hali iliyowashangaza wengi, msanii wa Bongo Fleva aliyepata matatizo na marehemu lakini yeye akapona, Mgaza Pembe ‘M 2 THE P’ aliibuka kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro ambako mwili wa marehemu ulikuwa ukiagwa.
Baadhi ya watu waliomtambua msanii huyo walionekana kumshangaa sana huku wakihoji ametua lini kutoka Sauzi.
M 2 The P alishindwa kuhimili wakati anapita kwenye mwili wa marehemu, alimwaga machozi, hali iliyosababisha waombolezaji wawili kumshika kulia na kushoto na kumtoa eneo hilo.

MAVAZI YAKE SASA!
Kikubwa kilichoibua maswali kutoka kwa waombolezaji ni jinsi msanii huyo alivyovaa. Wengine waliamini vaa yake ilisababishwa na kutaka kujificha watu wasimtambue. Pia wapo waliodai inawezekana alitoroka huko Sauzi.
Alivaa suruali ya ‘jinzi’, fulana ya mikono mifupi, miwani na kofia kubwa licha ya
hali ya hewa Morogoro kuwa si ya baridi sana kiasi cha kuvaa hivyo.

5. KUMBE MAREHEMU ALITUMIWA FEDHA SAUZI
Tofauti na mashabiki wake walivyoamini kuwa marehemu alikuwa akipiga fedha ndefu Sauzi na kuzituma Bongo kwa wanafamilia, mmoja wa ndugu zake alibumburua siri kuwa kuna wakati hali ilikuwa mbaya hadi ikabidi amtumie shilingi laki moja na nusu.
“Watu wanadhani labda Albert (Ngwea) alikuwa mambo safi muda wote Afrika Kusini kama vijana wengi wanavyoamini. Si kweli kuna wakati kabisa alikuwa akinipigia na kuniambia hali ilivyokuwa mbaya,” alisema ndugu huyo kwa sharti la kutotajwa gazetini.

Saturday, June 1, 2013

MSANII J-MARTINS AFUNGA PINGU ZA MAISHA

  Msanni na Producer toka Nigeria,Joshua Kalu Okwun aka J. Martins amefunga ndoa na longtime girlfriend,Nnezi Mbila jana January 2... thumbnail 1 summary

 

Msanni na Producer toka Nigeria,Joshua Kalu Okwun aka J. Martins amefunga ndoa na longtime girlfriend,Nnezi Mbila jana January 2,2012
J. Martins alifanya sherehe ya kimila pande za Ohafia,Abia State ambayo ilihudhuriwa na wanafamilia,marafiki wa karibu
J. Martins ni mmoja kati ya majembe yaliyowaweka wasanii P-Square kwenye ramani ya muziki duniani coz amefanya production asilimia kubwa ya hit songs zao na mpaka yeye mwenyewe kuamua kutoka kivyave kwa hits kama Oyoyo,Iva,Jukpa nk