Wednesday, March 27, 2013

WEKA MAZINGIRA SAFI KABLA MECHI..

Habari za siku wapenzi wasomaji wa Blog hii ya kona ya Mahaba.. Poleni sana na mihangaiko ya hapa na pale... Leo katika ukurasa wetu... thumbnail 1 summary



Habari za siku wapenzi wasomaji wa Blog hii ya kona ya Mahaba..
Poleni sana na mihangaiko ya hapa na pale...

Leo katika ukurasa wetu huu tutaangalia ni jinsi gani unaweza kuandaa mazingira bora kabla ya mechi(kufanya mapenzi).

Suala la kufanya mapenzi linahiitaji umakini na maandalizi mazuri..
Katika karne hii, watu wanayachukulia mapenzi kama sehemu ya kukidhi haja zao, hasa kiuchumi..

Kama kweli unajua kupenda na una mapenzi ya dhati kwa yule umpendae, fuata maelezo haya ili ufurahie mapenzi yenyewe...

1:WEKA MAZINGIRA SAFI.
Kwa siku hiyo ambayo unajua utakuwa na mwezi wako, jitahidi kuandaa mazingira ya ndani mwako yawe katika hali ya usafi..

Kibadilishe chumba kiwe na muonekano mpya.

2: TANDIKA MASHUKA YENYE MVUTO.
Baada ya kumaliza usafi, hakikisha kitandani kwako umetandika mashuka yenye maua au rangi zenye mvuto, hasa zile zenye ujumbe wa mapenzi..

3: Hakikisha chumbani kwako panapatika hewa safi ya kutosha..

JINSI YA KUMUANDAA MPENZI WAKO KABLA YA MECHI.

Kitu chochote ukitaka ukifanye ukiwa na raha,ni lazima ukiandae vizuri.. Katika suala la mapenzi, watu wengi wameshindwa kufikia kil... thumbnail 1 summary



Kitu chochote ukitaka ukifanye ukiwa na raha,ni lazima ukiandae vizuri..

Katika suala la mapenzi, watu wengi wameshindwa kufikia kilele cha raha kwa kutoelewa ni jinsi gani wawaandae wapenzi wao..
Tatizo hili lipo pande zote wanaume na wanawake..

Lakini kwa kiwango kidogo wanaume wanajitahidi kuwaandaa wapenzi wao kabla ya kuingia uwanjani.
Baadhi yao wanatambua sehemu za kuamsha hisia za wapenzi wao na wengi hawajui kabisa..

Mnapoandaana vizuri kabla ya mechi kuna wasaidia wote kuingia uwanjani huku akili na mwili vimechangamka kwa hisia kali za mahaba..

Kwa mwanamke inamsaidia asiweze kuchubuka wakati wa tendo kwa sababu sehemu zake za siri zitakuwa tayari zimelainika..
Pia huwasaidia kusogeza hisia zao karibu kwani wanawake wengi hisia zao huwa ziko mbali, ndio sababu wengi wao huwa hawafikii mshindo kwa sababu ya kukosa wanaume wanaojua kuandaa vizuri.

JINSI YA KUMUANDAA MPENZI WAKO:

Potezeni saa moja mkiwa katika maongezi ya kimahaba.,huku mkiwa mmekaa 0 distance.

Taaratibu mikono yenu ianze kutembea kwenye mwili wa kila mmoja.
Hakikisha inafika kila sehemu ya mwili wa mpenzi wako.

Kutanisheni midomo yenu, ndimi zenu zikutane, taaratibu nyonyaneni kwa zamu..

Kila mmoja apenyeze mkono wake na ashike sehemu za siri za mpenzi kwa dakika 5 zinatosha kabisa..

Penyeza ulimi wako masikioni kwa mpenzi wako..
Uuzungushe taaratibu huku ukimpumulia hewa pole pole..

Shika chuchu za mpenzi wako kwa ncha ya vidole,taaratibu zifinyefinye bila kumuumiza.
Unaweza pia kutumia ulimi..

Kumbuka usiwe na haraka katika kumuandaa mpenzi wako...

Naomba kwa leo niishie hapa,mengine tutajifunza kwenye mada zingine...

Tuesday, March 26, 2013

ALIYEMGONGA TRAFIKI NKO AFIKISHWA MAHAKAMANI

</..more..> Simbo  akitolewa selo. Akiingizwa mahakamani.   Akisubiri kusomewa mashitaka. Akiteta jambo na Is... thumbnail 1 summary


</..more..>
Simbo  akitolewa selo.
Akiingizwa mahakamani.
 Akisubiri kusomewa mashitaka.
Akiteta jambo na Issa Mnally (mpigapicha na mwandishi wa magazeti ya Uwazi, Ijumaa, Risasi, Amani na Championi) ndani ya mahakama kabla ya hakimu kuwasili.
Waandishi wa habari wakimpiga picha (Simbo) wakati akiingia mahakamani.
Akiongea jambo na wakili wake (mwenye koti jeusi) mara baada ya kesi kuahirishwa.
 
Akiondoka eneo la mahakama mara baada ya kesi kuahirishwa akiwa na wakili wake.
Jackson  Simbo  anayedaiwa kumgonga kwa gari marehemu trafiki Elikiza Nko wiki iliyopita maeneo ya Bamaga-Mwenge  jijini Dar es Salaam amepandishwa kizimbani leo katika mahakama ya Wilaya ya Kinondoni. Mshitakiwa huyo ameachiwa kwa dhamana hadi kesi hiyo itakapo tajwa tena Aprili 15 mwaka huu

Thursday, March 21, 2013

Wednesday, March 20, 2013

LWAKATARE ARUDISHWA RUMANDE, MBWA WAWATULIZA WAFUASI WA CHADEMA

LWAKATARE ARUDISHWA RUMANDE, MBWA WAWATULIZA WAFUASI WA CHADEMA Wakili anayemtetea Wilfred Lwakatare, Peter Kibatara (kulia), akimueleza... thumbnail 1 summary

LWAKATARE ARUDISHWA RUMANDE, MBWA WAWATULIZA WAFUASI WA CHADEMA

Wakili anayemtetea Wilfred Lwakatare, Peter Kibatara (kulia), akimueleza jambo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.
Mbowe akiwaeleza wanahabari njama za serikali kutaka kukidhoofisha chama chake.

JE UNAZIFAHAMU FAIDA NA HASARA ZA MITANDAO YA KIJAMII

FAIDA NA HASARA ZA MITANDAO YA KIJAMII Ndugu mwana Teknohama, leo naomba tumalizie makala hii ya athari za mitandao ya kijamii katika ma... thumbnail 1 summary

FAIDA NA HASARA ZA MITANDAO YA KIJAMII

Ndugu mwana Teknohama, leo naomba tumalizie makala hii ya athari za mitandao ya kijamii katika maisha ya watu.
Pamoja na mambo yote tulozungumza katika matoleo yalopita, leo ntaongelea kwa kina faida na hasara za mitandao ya kijamii.
Faida za mitandao ya kijamii:
  •  Mitandao ya kijamii inawasaidia watu kutengeneza mahusiano mapya kati ya ndugu na marafiki na pia inaongeza mawasiliano kati ya mtu na mtu na hivyo kuboresha mahusiano
  • Mitandao ya kijamii sasa imefungua mlango mpya kabisa wa chombo kingine cha habari. Imewafanya watu waweze kutuma ujumbe mfupi wa maandishi bure, watu wameza kublogu kama hivi, michezo ya mitandaoni, watu wameweza kubadilishana picha na habari mbalimbali kupitia mitandao hii ya kijamii
  • Mitandao ya kijamii imesaidia kuwaleta watu pamoja wenye mitizamo inayofanana. Mitizamo ya kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni, kimapenzi, kimichezo n.k. Watu ambao wamekuwa na matatizo ya kuongea siku hizi wanajisikia raha sana kuwasiliana na watu kupitia mitandao ya kijamii. Imekuwa ni uwanja mzuri wa watu kujionyesha kwa kile alicho nacho moyoni mwake na kukifikisha kwenye jamii
  • Baadhi ya watumiaji wa mitandao hii ya kijamii wamekuwa wakiitumia kutafuta hata kazi, wanafunzi wamekuwa wakiitumia kufanya majadiliano ya kimasomo mitandaoni, wanaharakati wametumia majukwaa ya mitandao ya kijamii kukutana na kuendesha harakati zao mitandaoni. Vyuoni hususai wamekuwa wakiendesha harakati zao kupitia mitandao ya kijamii. Tulishuhudia majuzi tu kwenye mgomo wa madaktari pale ambapo serikali ilipopiga marufuku mikutano ya madaktari, madaktari walibadilisha upepo wa mikutano ya uso kwa uso na kurudi kuwa mikutano ya mitandaoni
  • Baadhi ya watu wameitumia mitandao ya kijamii kupunguza misongo ya mawazo kwa kuwasiliana na watu mbali mbali na kujikuta wamefarijika katika matatizo walonayo. Wataalamu wa saikolojia wanashauri mtu anapokuwa na matatizo ni vema akaishirikisha jamii ili kupunguza mzigo wa kuchukua matatizo peke yake.
  • Mitandao ya kijamii kwa sasa imekuwa ikipanua wigo wake wa mawasiliano kutoka kuwa mitandao ya kijumla  na kuwa bayana zaidi. Kwa mfano watu wamekuwa wakitengeneza makundi ya fani fulani fulani ambapo inawasaidia wataalamu wa fani hiyo kukutana pamoja mtandaoni na hata kuongeza wigo wa kukutana uso kwa uso. Na hii imesaidia watu ambao wamekuwa wanataka kuingiza kwenye makundi ya fani hizo waweze kujumuika nao pamoja

Hasara za mitandao ya kijamii:
  • Mitandao ya kijamii imewafanya watu kutumia muda mwingi kuwasiliana mitandaoni na kuwafanya kuwa  wazembe sana kuwasiliana uso kwa uso.
  • Vijana wengi wanaoibukia kwa sasa hasa wenye umri kuanzia miaka 13 wako kwenye wakati mgumu sana kuathirika na matumizi ya mitandao ya kijamii. Kwanini nasema haya? Vijana wengi hawajui kwamba taarifa mbali mbali wanazoziweka mitandaoni ni taarifa mbazo zinaonekana  hata kama zikifutwa taarifa hizo zinaweza zikapatikana tu. Pamoja na kwamba mpaka sasa hakujawa na uhakika wa taarifa fulani kupatikana baada ya miaka fulani ijayo. Kwa hiyo utoaji mwingi wa taarifa za mtu binafsi inaweza kabisa kumfanya mtu kuwa muhanga wa mapenzi au wizi wa fedha na ujangiri mbali mbali mitandaoni. Watu wanatumia taarifa hizo kufanya uharifu. Kwa hiyo vijana wanatakiwa kuwa makini na taarifa zao wanazoziweka mitandaoni. Hii inaweza kusababisha hata mtu kufukuzwa kazi kama mtu anaweza kutoa taarifa fulani za mwajiri ambazo zinaweza kuleta mkanganyiko kwenye taasisi fulani.
  • Toleo lililopita nilizungumzia jinsi ilivyo ngumu kutambua utambulisho wa mtu. Baadhi ya mitandao ya kijamii imekuwa na desturi ya kuthibitisha utambulisho wa mtu. Kwa mfano, Takwimu zinaonyesha kuwa mtandao wa kijamii wa Facebook umekuwa na watumiaji zaidi ya milioni 700. Lakini nani anaweza kulithibitisha hilo maana kuna mtu unamkuta ana akaunti zaidi ya moja! Wakati mwingine mtu ni mwanaume lakini amefungua akaunti yenye utambulisho wa mwanamke! Hii inaleta mkanganyiko sana kwenye utambulisho wa watumiaji wa mitandao ya kijamii.
  • Muda wa kukutana uso kwa uso kwa ajili ya kubadilishana mawazo na kujichanganya na watu umepungua sana kwa sababu ya ongezeko la watu kutumia muda mwingi sana kwenye mitandao ya kijamii. Wazazi wamekuwa na muda mchache wa kubadilishana mawazo na watoto wao kwa kuwa watoto wao wamekuwa wako bize mitandaoni, wapenzi nao wamekuwa na muda mchache wa kubadilishana mawazo kwa kuwa kila mtu yuko bize kivyake mtandaoni!
  • Utafiti mmoja ulionyesha kwamba theluthi mbili ya wafanyakazi wenye akaunti za facebook huzitumia akaunti zao kubadilishana mawazo na watu mitandaoni kwenye muda wa kazi! Kwa maneno mengine wafanyakazi hawa wanaiba muda wa mwajiri wao! Kuna baadhi ya ofisi hasa za binafsi hapa Tanzania wenyewe wamekuwa wakiondoa mitandao ya kijamii kwenye mitandao ya ofisi zao zinazounganisha wafanyakazi na Intaneti. Changamoto ambayo ofisi hizi inazipata kwa sasa ni ongezeko kubwa la watu kutumia simu za mikononi, pamoja na tablets kuweza kuwasiliana kwenye mitandao ya kijamii kitu ambacho si rahisi kumzuia mtu kuwaisiliana kwenye mitandao ya kijamii. Ofisi za serikali hakika wamekuwa na changamoto kubwa sana kwa wafanyakazi wao wanaotumia mitandao ya kijamii kwani utendaji wao kazi hakika umepungua kwa sababu watu wanatumia muda mwingi sana kwenye mitandao ya kijamii wakati wa kazi.
Hii ndiyo Teknolojia yetu

kama una maoni yoyote juu ya hili naomba unitumie ujumbe wako ktk barua pepe zuberiamiri@gmail.com

Tuesday, March 19, 2013

Wednesday, March 13, 2013

TAARIFA KUTOKA TFF: WACHEZAJI 23 WAITWA STARS KUIKABILI MOROCCO, SEMINA ELEKEZI COPA COCA-COLA KUFANYIKA MACHI 19

TAARIFA KUTOKA TFF: WACHEZAJI 23 WAITWA STARS KUIKABILI MOROCCO, SEMINA ELEKEZI COPA COCA-COLA KUFANYIKA MACHI 19 Kocha Mkuu wa Taif... thumbnail 1 summary

TAARIFA KUTOKA TFF: WACHEZAJI 23 WAITWA STARS KUIKABILI MOROCCO, SEMINA ELEKEZI COPA COCA-COLA KUFANYIKA MACHI 19

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen.
Release No. 044
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Machi 13, 2013
WACHEZAJI 23 WAITWA STARS KUIKABILI MOROCCO
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametaja wachezaji 23 watakaoingia kambini Jumamosi (Machi 16 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mechi ya mashindano dhidi ya Morocco.
Mechi hiyo ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani nchini Brazil itachezwa Machi 24 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Kocha Kim, wachezaji wa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager wanatakiwa kuripoti kambini katika hoteli ya Tansoma, Machi 17 mwaka huu.
Wachezaji walioitwa ni makipa Juma Kaseja kutoka Simba ambaye pia ndiye nahodha wa Stars, Aishi Manula (Azam), Hussein Shariff (Mtibwa Sugar) na Mwadini Ally (Azam). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Nassoro Masoud Cholo (Simba) na Shomari Kapombe (Simba).
Viungo ni Salum Abubakar (Azam), Athuman Idd (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Khamis Mcha (Azam), Frank Domayo (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar).
Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Simba), Simon Msuva (Yanga), na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Mbali ya Kim, benchi la ufundi la Taifa Stars linaundwa na Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Tasso (Meneja), Dk. Mwanandi Mwankemwa (Daktari wa timu), Frank Mhonda (Mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).
SEMINA ELEKEZI COPA COCA-COLA KUFANYIKA MACHI 19
Semina elekezi kwa ajili ya michuano ya Copa Coca-Cola 2013 itafanyika Machi 19 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Washiriki wa semina hiyo wanatakiwa kuripoti Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) siku moja kabla (Machi 18 mwaka huu).
Washiriki hao ni makatibu wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya Tanzania Bara na Zanzibar. Pia waratibu wa mikoa wa mashindano ya Umoja wa Michezo wa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA).
Barua za mwaliko kwa ajili ya semina hiyo tayari zimetumwa kwa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa.