30 January 2014 Share this history on : digg Dereva wa boda boda Aliyejulikana kwa jina Bw Cheni Abed amef...
1:06 AM
Dereva wa boda boda Aliyejulikana kwa
jina Bw Cheni Abed amefariki dunia baada ya kugongana na baiskeli huku
dereva wa baiskeli hiyo ambaye pia alimpakia mwanaye wakiwa salama
salmini.
Cheni ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Mchuma
kata ya Kichangani mkoani hapa alipoteza maisha baada ya kugongana na
baiskeli hiyo na kuangukia kichwa kwenye makutano ya barabara za
Msamvu,Mafisa,Mwembesongo huku dereva wa baiskel hiyo ambaye alimpakia
mwanye wakisalimika kwenye tukio hilo.
Kufuatia mazingira ya tukio hilo
familia ya dereva boda boda huyo iliamua kusafiri hadi wilaya ya
mvomero kwenda kwa mganga wa kienyeji kuchunguza mazingira ya kifo
hicho ambapo Sangoma Hamis Masai mkazi wa kijiji cha Changarawe kata
ya Mzumbe Wilaya ya Mvomero mkoani hapa alimueleza baba wa mzazi wa
marehemu huyo Bw Abed Shabani kwamba mama yake mzazi ndiye alimuua
mjukuu wake huyo kwa kumchukua msukule na kwamba Sangoma huyo
alimhakikishia Mzee Shabani kwamba alikuwa na uwezo wa kumrejesha dunia
mwanye huyo aliekuwa nguvu muhimu kwenye familia hiyo.
Kufutia kauli hiyo Mzee Shabani aliludi
Morogoro mjini na kusitisha mazishi ya kijana wake kwa siku nne
akisubiri mganga huyo amfufue, kufuatia taarifa hizo majirani ambao
yatari walishaanza kutoa msaada wa kuchimba kaburi na kuchanga michango
ya mtaa walizuiwa kufanya shughuri hizo kwa maelezo kwamba Cheni
angefufuliwa. Habari za kufufuka kwa boda boda huyo
zilizagaa kwa kasi kubwa kama kile kimbunga cha sunami na kwamba siku
ya nne aliyohadi mganga huyo kumfufua boda boda huyo ilipofika umati wa
watu kutoka kona zote za mji wa morogoro walifika nyumbani kwa mzee
Shabani akiwemo wmandishi wa habari hizi kwa lengo akushuhida maajabu
hayo.
Familia hiyo na wananchi hao walisubiri
toka saa mbili asubuhi hadi saa moja usiku bila kushuhudi boda boda
huyo akifufu liwa na kwamba Sangoma huyo alipoulizwa na familia hiyo
alidai kwamba kuna mashariti yalivunjwa na familia hiyo hivyo asingewe
tena kumfufua marehemu wao na kwamba baada ya kauli hiyo watu
walitawanyika na kurudi siku iliyofuta kumzika boda boda huyo.
Katika mazishi hayio kuliibuka mambo
kadhaa ambapo miongoni mwa mwambo hayo ni mashekhe wote wa kata ya
kichanga kugoma kwenda kumsalimi marehmu huyo wakiitaka familia hiyo
kwenda kumwita mganga huyo wa kiennyeji wanayemuami aje kumsalia
marehemu wao.
Familia hiyo baada ya kuona viongozi
hao wa dini wamevuta 'Hend Breck' wameamu kukodi boda boda na kwenda
kumfuta shekh Mageta ambaye ana undugu na familia hiyo na kwamba kwenye
mawaidha yake Shekh Mageta akiipiga madogo familia hiyo kwa kuabudu
mamboya kishirikina.
"Nimepata ahabari mashekh wenzangu wa
eneo hili wamesusia kuja kwenye msiba huuu kwa mambo yetu ya kijinga ya
kuabudu ushirikina kijana wetu amekufa kwa ajari na amenguaki kiichwa
damu mwingi zimetoka leo mnaenda kuangua kwa mganga kuchunguza kifo
chake na mnadanganywa eti mganga huyo naweza kumfufua mtu mbona
ameshinwa kumfufua naomba sikunyingine msiludia jambo hili" alisema
Shekhe mageta kwwnye mawaidha yake.
Mwenyekiti wa taa huo wa chuma Bw
Nathanael Chacha ambaye alikiri kupokea taarifa za familia hiyo
kumfufua kijana wao alimu kuwaambia wajumbe wake waliokuwa kwenye zoezi
la kuchanga pesa za pole kuacha zoezi hilo.
Jambo la tatu lililojiri kwenye msiba
huo ni kwamba kwenye acouti ya simu ya marehmu kulikutwa pesa taslimu
shilingi laki sita na kwamba dada za marehmu walihangaika kuzitoa pesa
hizo bila mafanikia baada ya kushindw akuitambua namba ya siri ya
marehmu huyo licha ya kujari kuweka namba ya siri ya mwaka wa kuzaliwa
wa maremu huyo.
Baba mzaza wa marembu Mzee Abed Shabani
alipohojiwa na mtandao huu alikiri simu ya mwanayen huyo kuwa na kiasi
hicho cha fedha na kuda kwamba wanashindw akuzitoa baada ya
kutoitambua namba ya siri,habari ambazo mtandao huu umezinasa zilidai
kwamba mchumba wa boda boda huyo ambaye ameza naye mtoto mmoja ndiye
pekee nayejua namba za siri za simu ya mpenzi wake na kwamba kuna
habari zinadai kwamba wifi zake kwa sasa wamemficha jambo hilo naye
amedai kwamba kamwe hawezi kuwataji namba hizo za siri mapka
atakapohakikishiwa mgeno wa fedha hizo yeye na mtoto wake.
mwendezo wa tukio hili kwa maaba ya
picha za mazishi utawajia kesho hivyo usikose kutemebea mtandao huu
kujua mengi kujuu ya tukio hili ikiwemo ya bibi huyo wa marehmu
aliyetumia uchawi naye kufariki duni kwa Sangoma huyo