Saturday, August 31, 2013

NANDO ATIWA MBARONI KWA KASHFA YA KUIBA CAMERA NDANI YA JUMBA LA BBA...!

    Nando  ameendelea  kuitia  aibu  Tanzania  baada  ya  kukumbwa  na  kashfa  mpya  ya  wizi  wa  kamera  ndani  ya  j... thumbnail 1 summary

 

 


Nando  ameendelea  kuitia  aibu  Tanzania  baada  ya  kukumbwa  na  kashfa  mpya  ya  wizi  wa  kamera  ndani  ya  jumba  la  big  brother.

Wizi  huo  unadaiwa  kutendeka  baada  ya  Nando  kualikwa  kushiriki  fainali  za  Big brother  ambapo Dillish aliibuka  mshindi  wa  shindano  hilo.....

Baada  ya   wizi  huo, kamera  za  jumba  hilo  zilimuumbua.Nando  alikamatwa  na  kuamriwa  airejeshe  camera  hiyo.

Wednesday, August 28, 2013

MTANZANIA MWINGINE AKAMATWA NA KILO TATU ZA MADAWA YA KULEVYA DUBAI

  Mwanamke Mtanzania aliyekamatwa na dawa za kulevya Dubai baada ya kutiwa nguvuni. *Yana thamani ya zaidi ya shilingi bilion... thumbnail 1 summary

 

Mwanamke Mtanzania aliyekamatwa na dawa za kulevya Dubai baada ya kutiwa nguvuni.

*Yana thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.3
*Adai mzigo huo ni wa rafiki wa mumewe aliyempatia amletee Tanzania
*Alikuwa anatoka nchini Brazil kwa mapumziko ya miezi mitatu
Mwanamke mmoja ambaye ametambulika kuwa ni Mtanzania amekamatwa kwenye Uwanja wa Ndege Dubai akiwa na kilo tatu za dawa za kulevya aina ya Cocaine zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.3. Mwanamke huyo aliyekuwa anatoka nchini  Brazil kwa mapumziko kuja Tanzania baada ya kuhojiwa na maofisa wa polisi alidai kuwa rafiki wa mumewe ndiye aliyempa mzigo huo na  kumuomba amletee Tanzania.
Alieleza kuwa mumewe ndiye aliyemponza  baada ya kumuandalia safari ya Brazil kwa mapumziko ya miezi mitatu ndipo rafiki wa mumewe akamuomba amletee mizigo yake hiyo ambayo imemtia hatiani.

SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA,NI ZAMU YA MAWAZIRI SASA...

  Imezoeleka kwa raia wa kawaida kupekuliwa kwenye maeneo ya usafiri ili kuhakikiwa wasije kusafiri na vitu vya  hatari ikiwemo... thumbnail 1 summary

 


Imezoeleka kwa raia wa kawaida kupekuliwa kwenye maeneo ya usafiri ili kuhakikiwa wasije kusafiri na vitu vya  hatari ikiwemo silaha na madawa ya kulevya, huku viongozi wakipita ‘free’ lakini sasa Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe amebadili kibao.

Mwakyembe amebadili kibao hicho katika kipindi ambacho kuna tuhuma kwamba miongoni mwa waheshimiwa wanaounda Baraza la Mawaziri linaloongozwa na Rais Jakaya Kikwete ‘JK’, wapo wenye tabia ya kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya.
Kibao cha sasa kinasomeka kwamba ni zamu ya mawaziri wa JK wanaotajwa kujihusisha na uuzaji wa unga, kwa hiyo watakapokuwa wanasafiri kwenda kokote, iwe ndani au nje, lazima wakaguliwe na wakikutwa na ‘mzigo’ wataumbuka.



Tafsiri ya agizo la Mwakyembe alilolitoa wiki iliyopita kuwa viongozi wote watakuwa wanakaguliwa hususan watakapokuwa wanasafiri kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), limetafsiriwa na wajuzi wa mambo kwamba alilitoa kisayansi ya intelijensia.
“Kama Mwakyembe angesema mawaziri wanaotuhumiwa wakaguliwe, ingeleta picha mbaya na asingekamatwa mtu. Ameagiza viongozi wote wakaguliwe ili kuweka usawa. Alitumia akilia sana katika tamko lake,” alisema mwanaharakati wa madawa ya kulevya nchini, Mbena Nyiboma.
Mwakyembe alisema, ili kuhakikisha ‘uhuni’ wa kusafirisha madawa ya kulevya unakoma, viongozi wote watakaguliwa, isipokuwa Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Spika wa Bunge na Jaji Mkuu.

Waziri Mwakyembe akielezea jinsi madawa ya kulevya yanayopitishwa uwanja wa ndege jijini Dar.
KILIO KUHUSU MAWAZIRI WA JK
Mawaziri, wabunge, mabalozi na viongozi wengine wa kitaifa, wana hati za kusafiria za kidiplomasia (Diplomatic Passport), kwa hiyo hupita katika milango ya watu mashuhuri (VIP) bila kukaguliwa.
Kutokana na hali hiyo, zipo tuhuma za muda mrefu kwamba baadhi ya mawaziri, mabalozi hata wabunge, wamekuwa wakitumia fursa hiyo vibaya kwa kusafirisha au kutumiwa kusafirisha madawa ya kulevya katika mabegi na ‘briefcase’ zao.






Taarifa za mitandao ya kijamii zilianza muda mrefu, baadhi ya mawaziri, wabunge na wafanyabiashara wenye heshima kubwa nchini, wakitajwa waziwazi kwa majina kuwa wanatumia ‘u-VIP’ wao vibaya, kusafiri na madawa ya kulevya katika mabegi yao.
Hivi karibuni, zipo barua (japo uhalali wake bado ni kitendawili) ambazo inadaiwa kuandikwa na wafungwa wa kesi za madawa ya kulevya Hong Kong, China, zilizoelekezwa kwa JK, zikitaja vigogo wa biashara hiyo haramu na miongoni mwa watajwa wamo mawaziri na wabunge.

Mbwa wakiwa kazini.
MBUNGE ALIVYOWAWASHIA MOTO MAWAZIRI
Katika vikao vya Buge la Bajeti 2013-2014, mwaka huu, Mbunge wa Mwibara (CCM), Kangi Ligora, aliwawashia moto mawaziri wa JK, akidai kwamba baadhi yao ni wauzaji wakubwa wa madawa ya kulevya.
Bila kumung’unya maneno, Kangi alisema kuwa tatizo hilo ni kikwazo kwa maendeleo ya uchumi wa taifa na akataka mawaziri wauza unga wadhibitiwe kwa usalama wa nchi.
Kangi, aliyasema hayo wakati akichangia mjadala wa hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2013/2014 na akataka Kamishna wa Madawa ya Kulevya nchini naye awajibishwe kwa sababu ameonesha udhaifu wa kimapambano dhidi ya wauza unga.
Aliongeza kuwa serikali inawajua wauzaji wakubwa wa madawa ya kulevya, lakini inashindwa kuwakamata na kuwafikisha mahakamani kwa sababu ya rushwa, kwani watendaji wengi wanahongeka.

WAZIRI MKUU AKATOA KAULI YAKE
Kufuatia hoja ya Kangi, Mbunge wa Tumbe (Cuf), Rashid Abdallah, alimuuliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, swali la papo kwa papo, akimtaka atoe ufafanuzi kuhusu tuhuma za mawaziri kujihusisha na baishara ya madawa ya kulevya.
Pinda, akimjibu Rashid, alikanusha tuhuma hizo, zaidi alimwomba Spika Makinda amtake Kangi ataje mawaziri wanaofanya biashara hiyo haramu.





MWAKYEMBE AMETHUBUTU
Uamuzi wa Mwakyembe, umejikita katika kukata mzizi wa fitina kuhusu usafirishaji wa madawa ya kulevya nchini.
Kwa jumla, taifa limekuwa likipakwa matope kutokana na uzembe wa udhibiti wa usafirishwaji wa madawa ya kulevya hususan JNIA, matokeo yake watu wanakamatwa nje ya nchi na kuifanya Tanzania ionekane ni nchi inayokumbatia biashara hiyo.
Takriban miezi miwili iliyopita, wasichana wawili Watanzania, Agnes Gerald ‘Masogange’ na Melisa Edward, walikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo, Afrika Kusini wakiwa na kilo 150 za madawa ya kulevya aina ya Crystal Methamphetamine yenye thamani ya Shilingi bilioni 6.8.
Kitendawili cha namna shehena hiyo kubwa ya madawa ilivyoweza kupita JNIA bila kugundulika na mamlaka husika, kiliteguliwa na Mwakyembe hivi karibuni, alipotaja watumishi wa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege, waliohusika kusaidia kusafirisha mzigo huo kama walivyorekodiwa na Mfumo wa Kamera za Usalama (CCTV).
Baada ya kutegua kitendawili hicho, Mwakyembe amegeukia viongozi kwamba nao wakaguliwe ili kufanikisha mapambano ya jumla ya biashara ya madawa ya kulevya.

MUONEKANO MPYA WA SASA WA CRAZY GK....

    Baada ya kupotea kwenye muziki kwa muda mrefu sana Crazy Gk amerudi kwa kishindo na kuzindua wimbo wake mpya huku ak... thumbnail 1 summary

 

 



Baada ya kupotea kwenye muziki kwa muda mrefu sana Crazy Gk amerudi kwa kishindo na kuzindua wimbo wake mpya huku akisindikizwa na timu ya East Coast Team.
Sababu kubwa iliyopelekea King Crazy Gk kupotea kwenye game kwa muda mrefu ni kwamba msanii huyu alikuwa kwenye masomo akitafuta degree.


Read more: http://talkbongo.blogspot.com/2013/08/muonekano-mpya-wa-sasa-wa-crazy-gk.html#ixzz2dI7eFwbn

UZINDUZI WA VIDEO MPYA YA DIAMOND SERENA HOTEL!! KIINGILIO BURE LAKINI....!!

  Ni mazoea ambayo watu wake wamekua nayo kwamba akiwa na tukio kama hili basi ni lazima atalifanya kwenye mojawapo ya... thumbnail 1 summary

 


Serena hotel
Ni mazoea ambayo watu wake wamekua nayo kwamba akiwa na tukio kama hili basi ni lazima atalifanya kwenye mojawapo ya club za usiku Dar es salaam kama alivyokua akifanya mara nyingi lakini this time staa huyu anaelipwa ghali zaidi kwenye show zake ambae pia siku zake za kupumzika mara nyingi ni jumatatu au jumanne ameenda kwenye levo nyingine.
 
Diamond Platnumz kesho August 29 2013 anategemea kuitambulisha kwa fans wake video yake mpya kabisa ambayo picha zake zilisambaa kwenye mtandao ambapo ameishoot Afrika Kusini na hili tukio litafanyika kwenye hotel ya kifahari Dar es salaam… Serena.
 
Diamond mwenyewe anasema hakutakuwa na kiingilio kwenye uzinduzi huo lakini wataofika ni wale waliopewa mwaliko maalum kuingia kwenye hii hoteli maarufu ambayo ilizoeleka pia kuwahudumia mastaa wakubwa wa muziki kama Fabolous, Koffi Olomide na wengine lakini this time Diamond Platnums amekodi ukumbi alafu hataki watu walipe kiingilio, yani anaalika tu.
DIAMOND PLATNUM 2

Saturday, August 24, 2013

Msanii wa bongo movie/fleva apata ajali mbaya baada ya kugonga kalavati, analalamika kifua kinamuuma

  Msanii wa Bongo movie/bongo fleva, Hemedi a.k.a PHD alipata ajali jana usiku maeneo ya kijitonyama kisiwani, alipokuwa akito... thumbnail 1 summary

 



Msanii wa Bongo movie/bongo fleva, Hemedi a.k.a PHD alipata ajali jana usiku maeneo ya kijitonyama kisiwani, alipokuwa akitokea sinza kumshusha swahiba wake Gelly wa rhymes.

Hemedy ambae haijulikani alikuwa anaendesha under influence au la, alijikuta akivamia kalavati lililopo pembeni ya mtaro na kusababisha ajali hiyo iliyopelekea gari alilokuwa nalo kuwa nyang'anya'nga


Hemedi ameumia sana hasa kifua na kwa sasa anaendelea na matibabu na anaonekana kuwa na maumivu makali baada ya kuandia status hii

THANK GOD IM STILL ALIVE...NIMEUMIA SAANA KIFUANI ILA NAENDELEA NA MATIBABU..AHSANTE SANA @gellywarhymes kwa MAPENZI YAKO KWANGU NA WENGINE WOTE WALIONIPA POLE...#IN PAIN

Friday, August 23, 2013

MADAM RITA: "NAY WA MITEGO HANA PESA ZA KUNILIPA HATA NIKIMFUNGULIA KESI"

                                           Madam Rita  Mratibu wa shindano la Epic Bongo Star Search(EBSS) Rita Paulsen (Mada... thumbnail 1 summary

 




                                        Madam Rita

 Mratibu wa shindano la Epic Bongo Star Search(EBSS) Rita Paulsen (Madam Rita ) ameshangazwa na taarifa zilizoenea katika vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii ,kuhusiana na yeye kutaka kumfungulia mashtaka msanii Nay Wa Mitego ambaye anadaiwa kumchafua (defamation) katika wimbo wake mpya unaotamba sasa (Salamu Zao). Amesema hana mpango
wa kumfungulia mashitaka kwa kuwa hatakuwa na pesa za kumlipa kwa maana itakuwa kesi ya kumchafua na inaweza kumgharimu pesa nyingi.
.
Madam Rita ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano katika kipindi cha burudani cha The Strengo Saturday kinachorushwa na Radio Victoria fm kupitia 90.6 kilichopo Musoma, Mara. Ambapo mtangazaji wa kipindi hicho Patrick Derrick Mwankale alitaka kujua sababu kubwa ya EBSS kuhamishiwa katika kituo cha televisheni cha TBC1 ikitokea ITV na vipi kuhusiana na habari zilizopo za yeye (Madam Rita) kutaka kumfungulia Nay Wa Mitego kesi ya kumchafua . " unajua patrick nashangazwa sana na hizi taarifa zilizopo katika mitandao ya kijamii pamoja na vyombo vya habari, mimi sina mpango wa kumfungulia kesi mahakamani maana mimi ninajua anatafuta kick kupitia jina langu , anatafuta kuendelea kukaa katika soko la muziki kupitia jina langu, nikimfungulia kesi ya kunichafua mimi hatakuwa na hela ya kunilipa kabisa na kwanza nitakuwa napoteza muda wangu wa kusumbuana naye nakuzidi kumuweka juu zaidi. unajua mimi kwanza hata simfahamu, sijawahi kukutana naye, sijawahi hata kukaa nae na hapo ndipo nitalazimika kumtafuta ili nimjue, lakini kuhusu kumfungulia kesi siwazi kabisa maana hana hela ya kunilipa huyo" alisema Madam Rita

 Madam Rita akionekana kuumizwa zaidi na taarifa hizo, amesema , huyo msanii ni kati ya wasanii wasiojitambua kabisa wala kujielewi. Maana kabla ya kuimba chochote anatakiwa kufanya reasech ya kutosha na siyo kuropoka ujinga kujitafutia kick , kwa kuwa hata watanzania pamoja na wasanii wenyewe wanamshangaa kwa hayo anayosema na kuimba. Kila mtu anajua kuwa hela na zawadi zinazotangazwa zinatoka na siyo propaganda na kama ni swala la msanii kutokusikika au kuvuma baada ya yeye kutolewa na shindano hilo hiyo ni juu yake binafsi.

Pia alisema hakuna sababu kubwa sana iliyopelekea EBSS ya mwaka huu kuhamishiwa TBC1 zaidi ya maslahi ya kibiashara .Na pia ndio channel ambayo hivi sasa ina watazamaji wengi kutokana na ishu ya ving'amuzi kwasababu ITV kuna baadhi ya mikoa haikamati kwa sababu ya ishu hiyo ya ving'amuzi.

KAULI YA MWASITI KUHUSU ALICHOKISEMA NEY WA MITEGO KWAMBA KIGOMA ALL STARS IMEKUFA

    Leo hii msanii na muhasibu wa Kigoma All Stars,  Mwasit Almasi a.ka Mwasiti amezungumza juu ya tuhuma za rapper Ney wa mit... thumbnail 1 summary

 



 

Leo hii msanii na muhasibu wa Kigoma All Stars,  Mwasit Almasi a.ka Mwasiti amezungumza juu ya tuhuma za rapper Ney wa mitego kupitia wimbo wake "nasema nao" kuwa Kigoma All Stars imekufa.
 

  mwasitiamesema"Hahahaaa jamani, unajua mi siendi kujibu hizi mambo, mi sipendi hizo maneno maneno
kurushiana,lakini mi nataka watanzania wajue kitu kimoja, safari hii simjibu Ney, najibu watanzania kwasababu wao ndio wamepelekewa ujumbe, nawaambia watanzania kwamba Kigoma All Stars ni kampuni sio group ya mziki, kigoma all stars ni kampuni ya wanamziki, ingekuwa ni group wangekuwa wanatuona tunafanya kazi wote kila sehem sasa hivi, ile ni kampuni ya wanamziki ambao wanashughuli zao, huwezi kukuta hiyo group nzima iko kwenye  mkoa mmoja inafanya show mfano Fiesta, ni ngumu, ile mtu akipelekwa ni kazi yake binafsi , lakini tukimuhitaji kwenye kazi ya kampuni tutampata, kwahiyo hakuna kitu kinachoitwa kufa kwa kigoma all Stars, kigoma all stars ni kampuni ambayo kila mwana mziki ana share katika ile kampuni, kwahiyo ni ngumu kufa, kila mwanamziki amewekeza pale, kila mwanamziki anajua hapa nina changu kwahiyo ni yake"

Friday, August 16, 2013

FUTA DELETE KABISAAAAAA..

  Unapopokea ujumbe, katika simu yako au katika mtandao wowote ule wa kijamii na ikiwa ujumbe huo una lengo la kuhatarisha... thumbnail 1 summary

 



Unapopokea ujumbe, katika simu yako au katika mtandao wowote ule wa kijamii na ikiwa ujumbe huo una lengo la kuhatarisha  usalama, kuvuruga amani ama kurudisha maendeleo nyuma, ni vyema ukafuta na kudelete kabisa ujumbe huo usiusambaze. Hakikisha unafuta na ku delete kabisaa
Ungana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Katika kampeni ya FUTA DELETE KABISA.

SOMO LA KUJIFUNZA KUTOKA KWA ‘TRAFFIC’ FEKI

    Jana kulikuwa na taarifa za askari traffic feki aliekamatwa akisimamisha magari maeneo ya tabata kinyerezi, dar es salaam. Ime... thumbnail 1 summary

 



  Jana kulikuwa na taarifa za askari traffic feki aliekamatwa akisimamisha magari maeneo ya tabata kinyerezi, dar es salaam. Imekuwa ni habari iliyovuta hisia za wengi, na mengi yamezungumzwa kutokana na kitendo cha huyo mtu alieamua kuchukua maamuzi hayo.
TRAFICTRAFIC2
  Wengi wanasema ugumu wa maisha umemfanya jamaa kutafuta mbinu mbadala ya kujipatia kipato. Kuna wengine wanamshangaa kwa kujiamini kiasi hiko mpaka kuwa askari bandia.
  Ni hali ya kushangaza kwa kweli na kila mtu ana haki ya kushikwa na butwaa. Badala ya kuishia tu kushangaa na kuachia hapo kuna somo kubwa sana la kujifunza kutoka kwa huyu mtu.
  Huyu bwana ana nguo zote za traffic na mpaka kifaili cha kuwaandikia watu makosa, sawa huenda kavipata kwa njia za rushwa ama wizi ama kinginecho.
  Huyu bwana aliweza kufanya kila kinachofanywa na traffic wa kawaida bila kuhisiwa na mtu yeyote yule. Kilichomfanya akamatwe ni kutopiga salute kwa askari wa cheo cha juu ambae huenda hakumfahamu kwa sura(kama angemfahamu bila shaka angempa heshima yake)
  Huyu bwana hakutaka kukaa kariakoo wala ubungo wala tazara ama buguruni. Kajitafutia kaeneo kake ka ndani ndani, tabata kinyerezi na kuanza kula vichwa.
  Ukiangalia mambo yote yaliyofanywa na huyu traffic feki yametumia ubunifu mkubwa sana, amejifunza kwa makini matrafiki wanavyofanya na amechagua eneo ambalo sio rahisi kwake kujulikana.
  Niliwahi kuandika kila mtu ni mbunifu(soma; kila mtu ni mbunifu). Na somo kubwa tunaloweza kujifunza kwa huyu bwana ni kwamba ukiwa mbunifu unaweza kufanya chochote. Japo yeye kavuka mstari na kuvunja sheria.
  Sikuambii ujifunze kufanya uhalifu ili kujikimu na maisha yako. Usijaribu kufanya hivyo hata kidogo. Tumia ubunifu ulionao ambao hujaweza kuutumia bado kupata njia za kufikia malengo yako.
  Hakuna ambae sio mbunifu, tatizo ni wachache sana wanaotumia ubunifu wao. Anza na wewe kutumia ubunifu wako.

NGASSA ATAKIWA KUREJESHA FEDHA ZA SIMBA NA FIDIA JUU MILIONI 15 ILI ACHEZE YANGA, PAMOJA NA HAYO AFUNGIWA MECHI SITA KUANZIA KESHO NA AZAM HACHEZI

  Na Boniface Wambura, IMEWEKW3A AGOSTI 16, 2013 SAA 9:45 ALASIRI KAMATI ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka... thumbnail 1 summary

 



Na Boniface Wambura, IMEWEKW3A AGOSTI 16, 2013 SAA 9:45 ALASIRI
KAMATI ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imepitia usajili wa wachezaji wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom na kumuidhinisha Mrisho Ngasa kuchezea timu ya Yanga baada ya kukamilisha usajili wake.
Hata hivyo, Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa imebaini kuwa Ngasa alisaini mkataba mwingine Simba (katika kipindi ambacho alikuwa na mkataba na Azam) ambapo anatakiwa kurejesha fedha alizopokea (sh. milioni 30) pamoja na fidia ya asilimia 50 (sh. milioni 15) ya fedha hizo kwa Simba.
Rudisha Fedha za Simba; Ngassa ameamriwa kurejesha fedha za Simba SC na fidia juu,

Kamati pia imemfungia mechi sita za mashindano (kuanzia mechi ya Ngao ya Jamii), na anatakiwa awe amelipa fedha hizo ndani ya kipindi hicho cha kukosa mechi hizo. Akishindwa, hataruhusiwa kucheza hadi atakapolipa fedha hizo.
Kicheko baada ya kazi;Wajumbe wa Kamati ya Sheria Maadili na Hadhi za Wachezaji, Mawakili, Imani Madega, Alex Mgongolwa (Mwenyekiti, katikati) na Lloyd Nchunga kushoto wakiwa nje ya ofisi za TFF baada ya kikao.

Vilevile Kamati imepitia pingamizi zote zilizowasilishwa kuhusu usajili wa wachezaji, kukatiza mikataba ya wachezaji na kuzitaka klabu husika ziwe zimetatua masuala hayo hadi Alhamisi (Agosti 22 mwaka huu).
Kwa upande wa wachezaji wa kigeni, Kamati imeagiza wasiruhusiwe kucheza hadi watakapopata Hati za Uhamisho wa Kimataifa (ITC) pamoja na vibali vya kufanya kazi nchini (work permits).
Kamati hiyo itakutana tena Ijumaa (Agosti 23 mwaka huu) ili kupata ripoti za pingamizi ilizoagiza ziwe zimefanyiwa kazi hadi Agosti 22 mwaka huu na kutoa uamuzi kwa pande ambazo hazikuafikiana.
Wakati huo huo: Kamati ya TFF kwa kuzingatia mamlaka iliyonayo katika kifungu cha 10(6) cha Kanuni za Uchaguzi za TFF inasogeza mbele tarehe ya uchaguzi wa TFF kutoka Oktoba 20 mpaka Oktoba 26 na 27 mwaka huu.
Sababu za kusogeza mbele uchaguzi ni kutokana na ukweli kuwa Oktoba 20 mwaka huu uongozi wa TFF utakuwa na shughuli nyingi za maandalizi ya mechi ya Simba na Yanga, na hivyo haitawezekana kusimamia shughuli za Mkutano Mkuu wa Uchaguzi kwa wakati mmoja na mchezo huo.
Siku ya mwisho ya kampeni itakuwa Oktoba 25 mwaka huu. Ukiondoa  mabadiliko hayo ya tarehe ya uchaguzi wa viongozi wa TFF, ratiba ya mchakato wa uchaguzi na itabaki kama ilivyotangazwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF katika mkutano wake na waandishi wa habari Agosti 24 mwaka huu.
Pia Kamati imeamua kuwa uchaguzi wa Bodi ya Ligi utabakia kuwa Oktoba 18 mwaka huu kama ilivyopangwa awali.
Kamati imesema inaamini wahusika wote watapokea vizuri mabadiliko hayo na inasikitika kwa usumbufu utakaosababishwa na mabadiliko hayo.

ULE mwaliko uliobuma wa mastaa wa Bongo Muvi wa kwenda kufuturu ikulu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho K... thumbnail 1 summary

ULE mwaliko uliobuma wa mastaa wa Bongo Muvi wa kwenda kufuturu ikulu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete umeibua tafrani na kusababisha moto kuwaka ndani ya tasnia hiyo.




                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                          Baadhi ya mastaa hao wanatuhumiana kutapeliana fedha walizochangisha kwa ajili ya kukodi magari ambayo yangewabeba kutoka pale Viwanja vya Leaders, Kinondoni hadi ikulu iliyopo Magogoni, Dar. Akizungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa, mmoja wa wasanii hao alisema: “Baada ya kukusanyika pale Leaders (siku ya tukio) tuliamua kuchangishana kwa ajili ya kukodi magari ambayo yangetupeleka ikulu lakini wakati zoezi hilo likiendelea ndipo ulipokuja ujumbe kuwa safari hiyo imekufa baada ya Rais Kikwete kupata mgeni kutoka Marekani, Bill Clinton. “Sikuwa na shaka na taarifa zile za kuahirishwa kwa mwaliko wa kwenda kufuturu ikulu, nilitegemea kuwa kila mtu aliyechangishwa angerudishiwa fedha zake lakini hadi tunaondoka maeneo ya Leaders hakuna aliyerudishiwa.” Baada ya kupata maelezo hayo, gazeti hili lilimtafuta aliyekuwa mratibu mkuu wa mwaliko huo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ambapo aliposomewa mashtaka yake alikiri kutokea matatizo hayo huku akitupa lawama moja kwa moja kwa wachangishaji. “Muulize Muhogo Mchungu (Rajab Mkumbila) au Chiki (Salum) Mchoma, hao ndiyo watakupa jibu kamili,” alisema Steve Nyerere Kwa upande wake, Chiki alisema kuwa hapendi kuzungumzia suala hilo huku naye akimtupia mpira Muhogo Mchungu kuwa ndiye aliyekuwa na daftari la waliochangisha. Naye Muhogo Mchungu alipotafutwa na mwanahabari wetu alisema kuwa kama kuna mtu anadai fedha zake amtafute na si kulalamika kwenye vyombo vya habari.
.

Thursday, August 15, 2013

Thursday, August 15, 2013 | 11:38 PM Wakili Nassor Jumaa anayesimamia Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam nchini, Sheik... thumbnail 1 summary

Thursday, August 15, 2013 | 11:38 PM



Wakili Nassor Jumaa anayesimamia Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda (54) ambaye kwa sasa anakabiliwa na kesi mpya ya kufanya uchochezi katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amezungumzia leo hii majira ya saa 7 mchana nje ya viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar  es Salaam  ambapo  amesema kuwa amesikitishwa na hatua  ya vyombo vya dola kumuondoa Sheikh Ponda aliyekuwa amelazwa katika wodi ya Kitengo  cha Taasisi ya Tiba  ya Mifupa  na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu (MOI) alikokuwa akipatiwa matibabu na kisha kumhamishia katika gereza la Segerea.

Wakili Jumaa amesema amesikitisha na kitendo hicho kwani muda mfupi baada ya wakili mwandamizi wa serikali Tumaini Kweka kumaliza kumsomea Sheikh Ponda shitaka linalomkabili, Hakimu Hellen Riwa alitoa amri ya kukaa chini ya ulinzi Sheikh Ponda aendelee na matibabu.

Jumaa akasema ameshangazwa kuona leo, wanausalama wamemtoa Sheikh Ponda wodini na kumpeleka katika gereza la Segerea na kwamba atalazimika kurudishwa tena mahakamani siku kesi yake itakapojatwa Agosti 28 mwaka huu, ambapo upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

“Kwa kweli kitendo hicho kime nisikitisha na kunishitua sana… ila tunatafakari ni hatua gani za kisheria tutazichukua huko siku za usoni,”alisema Jumaa.
 Kwa upande wao familia ya Sheikh Ponda wamesema wanalaani kitendo kilichofanywa na serikali cha kumuondoa ndugu yao hospitalini huku akiwa anaendelea kupata matibabu.

Msemaji wa familia hiyo Is-haq Rashid, alisema kutokana na hali hiyo kama familia wanalirudisha suala la Sheikh Ponda kwa uongozi wa jumuiya na Taasisi za kiislamu kwa ajili ya hatua zaidi ya kuhakikisha kiongozi mwenzao anakuwa salama.

“Uporaji huu wa mgonjwa unazidi kutupa mashaka juu ya dhamira ya serikali hasa ikiwa tunalituhumu jeshi la polisi katika kumdhuru Sheikh,hatujui kwanini kila wakati wanafanya mambo yao kwa kuvizia kama mwanzoni tuliwaomba viongozi wenzie wawe na subira juu ya yaliyotokea sasa tunaachia hili walizungumzie wao.”alisema Is-haq.

Wakati huo huo taarifa zilizopatikana zinaeleza kuwa viongozi wa Jumuiya na Taasisi zaKiislamu  walikuwa katika kikao kizito cha kujadili hatua hiyo ya kuporwa kwa Sheikh Ponda akiwa katika matibabu

Wakati huo huo taarifa zilizopatikana zinaeleza kuwa viongozi wa Jumuiya na Taasisi zaKiislamu  walikuwa katika kikao kizito cha kujadili hatua hiyo ya kuporwa kwa Sheikh Ponda akiwa katika matibabu.
.

HALI HII NI HATARI...

Kadhia ya usafiri wa Noah: Abiria wakiwa wamepangwa hadi nyuma ya siti wakiwa kwenye usafiri huo kutoka  Mikumi kwenda Mjini M... thumbnail 1 summary



Kadhia ya usafiri wa Noah: Abiria wakiwa wamepangwa hadi nyuma ya siti wakiwa kwenye usafiri huo kutoka  Mikumi kwenda Mjini Morogoro, kama walivyokutwa leo na kamera yetu eneo la Kijiji cha Mangae, Wilaya ya Mvomero ,barbara kuu ya Iringa - Morogoro. Licha ya gari hizo kuruhusiwa kubeba abiria baadhi ya wenye magari hayo hawazingatii kanuni za usafirishaji kwa kujaza abiria wengi kinyume na sheria.
Abiria wanashuka, wengine wanaingia...
 
Mlango unafungwa
 
Haya, safari njema...
 

TANZIA:MPIGANAJI GRACEMO BAMBAZA AFARIKI DUNIA....

  . Mpiganaji Gracemo Bambaza (pichani) aliyekuwa mwandishi wa habari za michezo aliyekuwa akikitumia kituo cha Radio ... thumbnail 1 summary

 



.



Mpiganaji Gracemo Bambaza (pichani) aliyekuwa mwandishi wa habari za michezo aliyekuwa akikitumia kituo cha Radio cha wapo Radio cha Kurasini jijini Dar es Salaam /Pride Fm ya Mtwara na  kituo cha ABM ya  Dodoma na kufanya Mafunzo ya Habari akiwa katika masomo yake ya Diploma katika kituo cha Channel 10 amefariki Dunia jana Agosti 14, 2013.  
Marehemu alikuwa akisumbuliwa na Saratani ya Koo mpaka mauti yanamkuta katika Hospitali ya Ocean Road. Marehemu alizaliwa Mwaka 1973 Mkoani Kagera na amesafirishwa leo Agosti 15, 2013 kwenda Karagwe mkoani kagera kwa mazishi. Marehemu ameacha Mke na mtoto Mmoja .
Kwa Taarifa zaidi wasiliana na Dada wa Marehemu 
Mary Mihigo 
0713 64 49 41


.

Sunday, August 11, 2013

DANGURO LA UCHI LAFUMULIWA BUGURUNI DAR..... GHARAMA YA CHUMBA NI 1200/= ....KUMLIPA MALAYA NI 5000..

JUMBA linalodaiwa kutumika kuendesha shughuli za ukahaba limebainika kuwapo katika eneo la Buguruni, jijini Dar es Sa... thumbnail 1 summary


JUMBA linalodaiwa kutumika kuendesha shughuli za ukahaba limebainika kuwapo katika eneo la Buguruni, jijini Dar es Salaam.

Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima, umebaini kuwapo kwa jumba ambalo linatumika kama nyumba ya kulala wageni, ambako idadi kubwa ya makahaba hujazana na kuendesha biashara ya kuuza miili yao bila wasiwasi. 




Wasichana wanaofanya biashara hizo hutoza kiasi cha sh 5,000 kama huduma ya ngono na chumba kwa matumizi ya muda mfupi.

Biashara hiyo ambayo imeleta usumbufu mkubwa kwa wakazi wengi wanaopakana na nyumba hiyo, imekuwa

ikifanikiwa kutokana na kuwapo kwa baadhi ya askari polisi wanaodaiwa kuwalinda wasichana hao pamoja na mmiliki wa nyumba hiyo.

Nyumba hiyo inavyo vyumba vingi vinavyotozwa kiasi sha sh 1,200 kwa chumba pamoja na kondomu. Kadhalika wasichana wenye umri wa miaka 15, ni miongoni mwa wanaofanya biashara hiyo.

Mjumbe wa serikali ya mtaa wa eneo hilo, Amiri Banza, alikiri kuwapo kwa biashara hiyo, ingawa alisema wamejaribu sana kuzuia hali hiyo bila mafanikio: 

“Tumechoka na hii kadhia, tumeripoti kwa viongozi wa Kata hadi polisi lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa. Kama wakija polisi wanawakamata, halafu wanawaachia,” alisema.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi wa Ilala, Marietha Minangi alipoulizwa juu ya kuwapo kwa jumba hilo alisema hajui chochote.: “Mimi sijapata taarifa hizo na ndiyo kwanza ninakusikia wewe,” alisema.

Alipoulizwa kuhusu polisi kufika kwenye jumba hilo na kuchukua rushwa na kuondoka alisema: “Sina ushahidi, kama wapo polisi wanafanya hivyo ni kosa,” alisema Minangi na kuongeza kuwa polisi wanafanya doria maeneo hayo na mara kadhaa wamewakamata watu wanaojihusisha na vitendo hivyo na kuwafikisha mahakamani.

Friday, August 9, 2013

KUKAMATWA KWA MASOGANGE... VIGOGO WAWILI WABANWA...

  HABARI zilizochimbuliwa kwa undani zinadai kuwa tayari vigogo wawili waishio nchini wamebanwa na Jeshi la Polisi Ta... thumbnail 1 summary

 





HABARI zilizochimbuliwa kwa undani zinadai kuwa tayari vigogo wawili waishio nchini wamebanwa na Jeshi la Polisi Tanzania wakituhumiwa kumtuma Masogange kupeleka madawa ya kulevya nchini Afrika Kusini.

Agnes Gerald 'Masogange'  Kwa mujibu wa habari hizo, vigogo hao (majina tunayo) walidakwa wiki iliyopita kila mmoja kwa wakati wake na kuhojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi (Central), jijini Dar ambako walihojiwa kwa saa sita.
“Hawa vigogo walikamatwa wiki iliyopita na kuhojiwa kwa masaa sita, waliachiwa lakini waliambiwa wakihitajika tena wataitwa,” kilisema chanzo hicho.
Chanzo kikaongeza kuwa, licha ya kuhojiwa na kuruhusiwa kuondoka, vigogo hao, mmoja alinyang’anywa ‘paspoti’ yake huku mwingine akaunti zake za benki zikifungwa kwa muda usiojulikana.
Habari zinasema kuwa, kigogo ambaye akaunti zake zimefungwa amekuwa akihaha kila kukicha kuhakikisha zinafunguliwa kwa sababu hana njia nyingine ya kuingiza kipato.
Juzi, Ijumaa liliwasiliana na Kamanda wa Kikosi Maalum cha Kupambana na Madawa ya Kulevya, Godfrey Nzowa ili kujua uhakika wa madai hayo ambapo alisema:
“Sisi (polisi) tumekuwa tukifanya mambo yetu kwa siri kubwa, si rahisi kusema. Tukisema kunakuwa na ugumu kwa sababu mnaandika kwenye magazeti, matokeo yake uchunguzi unavurugika.
“Mfano wale wasichana (akina Masogange) waliokamatwa Afrika Kusini wamekuwa wagumu kuwataja waliowatuma kwa sababu hao waliowatuma ndiyo wanaowategemea kuwawekea dhamana.”
Agnes Gerald na mwenzake, Melisa Edward walikamatwa Julai 5, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo uliopo Kempton Park nchini humo wakiwa na madawa ya kulevya aina ya Crystal Methamphetamine yenye thamani ya shilingi bilioni 6.8.

#Fahamu: Kabla Ya Kuwa Star Wa Muziki, Linex Sunday Mjeda Aliwahi Kufanya Kazi Hii Huko Iringa

Msanii wa muziki wa kizazi kipya hapa Bongo, Linex Sunday Mjeda ameweka wazi kuwa, kabla ya kuwa staa wa muziki aliwahi kufanya kazi kama ... thumbnail 1 summary

Msanii wa muziki wa kizazi kipya hapa Bongo, Linex Sunday Mjeda ameweka wazi kuwa, kabla ya kuwa staa wa muziki aliwahi kufanya kazi kama ripota wa redio,kitu ambacho watu wengi walikuwa hawakifahamu.
Linex amesema kuwa aliwahi kufanya kazi hii kwa muda kidogo akiwa huko Iringa katika kituo kimoja maarufu cha redio, na amekanusha kuwa aliwahi kuchangayikiwa na kupoteza kazi hiyo kutokana na kuvuta Bangi.

Msanii huyu amesema yupo vizuri sana na ataendelea kuwapatia watu vile vitu wanavyovipenda kupitia kipaji chake kikubwa cha kuimba.

Thursday, August 8, 2013

FACEBOOK YASABABISHA MAGONJWA MAPYA YA KIDIJITALI SOMA HAPA BY CHEKA NA KITIME

Kutokana na matumizi makubwa ya Facebook tayari kumeanza kupatikana magonjwa ambayo yanatokana na hii kitu, katika semina niliyohudhu... thumbnail 1 summary

Kutokana na matumizi makubwa ya Facebook tayari kumeanza kupatikana magonjwa ambayo yanatokana na hii kitu, katika semina niliyohudhuria jana niliweza kufahamishwa baadhi ya magonjwa mapya kabisa yafuatayo;

1.LIKOSIS.
Huu ni ugonjwa ambao mgonjwa huwa ana ‘like’ kila status na picha yoyote atakayoiona mbele yake. Ugonjwa huu huwapata hasa wale ambao ndio kwanza wanaanza kutumia FB
2.LIKOPHOBIA
Huu ni ugonjwa wa kutoku ‘like’ kitu chochote, ugonjwa huu wanao sana masupastaa wa bongo, maana huwa na tatizo la kisaikolojia kuwa waki’like’ watashuka hadhi na kuwa watu wa kawaida
3.AIBUMIASIS
Huu ni ugonjwa wa kuionea aibu FB. Mtumiaji huingia FB labda mara moja kwa mwezi halafu anaona aibu kuingia tena mpaka mwezi unaofuata.
4. TAG SYNDROME
Ni ugonjwa ambao mwana FB anataka umtag kila picha anayoiona hata isiyomuhusu
5. HATE SYNDROME
Huu ni ule ugonjwa wa mwana FB ambapo yeye huweka status za ‘hate’ tu. I hate life. I hate haters, I hate Dar, I hate CCM, I hate CDM
6. REQUEST SYNDROME
Hapa ni ule ugonjwa wa mwana FB kurequest marafiki bila hata kuwa anawajua anataka tu aonekane anao wengi.
7. COMMENTOLARIA
Mwenye ugonjwa huu, hu comment kwenye kila status itakayotokea mbele yake, yanayomhusu na yasiyomhusu, mradi ka comment
8.MBULULATOSIS
Mwenye ugonjwa huu hucomment utumbo tu kila mara, status na mazungumzo yanaweza kuwa ni ya kuhusu ujio wa Obama, yeye ataweka tangazo la duka lake la simu, au ataulizia Kofi Olomide ana umri gani
 9. ADICTOMIOLOGY
Mgonjwa anaweza kuhisi kufa kama katimiza masaa 24 bila kuingia FB

DIAMOND NOMA SANA: ONA ALICHOKIFANYA SOUTH AFRICA ALAFU MSEME DIAMOND ANALOGA-HARD WORK PAYS BWANA

Bongo Flava Prince, Diamond Platnumz yupo nchini Afrika Kusini kishule na kikazi pia. Staa huyo wa Kesho ameshoot video ya wimbo wake mp... thumbnail 1 summary

Bongo Flava Prince, Diamond Platnumz yupo nchini Afrika Kusini kishule na kikazi pia. Staa huyo wa Kesho ameshoot video ya wimbo wake mpya ambao bado haujulikani ni upi mpaka sasa.
Hata hivyo tofauti na video zake za awali, hii mpya amekata kisu kirefu zaidi kwa kushoot na miongoni mwa gari yenye thamani zaidi duniani, Ferrari. Cha kufurahisha zaidi ni kuwa gari hiyo inayotengenezwa na Waitaliano, imewekewa namba za gari binafsi kwa kuandikwa ‘Platnumz’ na Wasafi’.
0b54d01efdd411e2bd3c22000ae90db5_7
Mafundi wa Afrika Kusini wakihakikisha plate ya Wasafi imekaa vizuri
0f7a71cefdef11e2999e22000a1f8afc_7
dd5ff8c8fdce11e2aa0322000a1fa408_7
Inaonekana hii, Diamond Platnumz aka Coca Boy amejiandaa kwenda international zaidi.
Picha: Babutale (Instagram)

Wednesday, August 7, 2013

SHOGA APOTEZA MAISHA BAADA YA KUFANYA MAPENZI NA WANAUME WATATU KWA AHADI YA DAU NONO....

  Hii  ni  picha  ya  shoga  toka Nigeria  ambaye  anadaiwa  kupoteza  maisha  ndani ya gesti baada  ya  kufanya  mapenzi  na  wan... thumbnail 1 summary

 
Hii  ni  picha  ya  shoga  toka Nigeria  ambaye  anadaiwa  kupoteza  maisha  ndani ya gesti baada  ya  kufanya  mapenzi  na  wanaume    watatu  kwa  ahadi  ya  dau  nono.....

Taarifa  zinadai  kwamba  shoga  huyo  alizidiwa  nguvu  na  wateja  wake  ambao  walimwingilia  kiasi  cha  kumtoa  kinyesi....

Kwa  mujibu  ya  mitandao  ya  kinigeria,  Kelele  toka  ndani  ya  chumba  alichokuwa  kijana  huyo  ziliwastua  wahudum  wa  Gest  hiyo   na  kuwalazimu  waite  polisi  wakidhani wamevamiwa....
  Taarifa  zinaendelea  kudai  kuwa  polisi  walipofika  eneo  la  tukio   walimkuta kijana  huyo  "akitema  utumbo  makalioni"  na  wateja  wake  walikuwa  wamekwisha  kimbia